Kocha Deschamps:Lakini Kylian atabaki kuwa Kylian siku zote, Ufaransa tupo tayari kwa Uingereza

NA DIRAMAKINI

KOCHA wa Ufaransa, Didier Deschamps amezungumzia pambano lijalo la timu yake dhidi ya Uingereza katika mkutano na waandishi wa habari.

Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps. (Picha na AP).

Les Bleus ndio mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, lakini wanakumbana na timu ya Uingereza iliyo katika hali nzuri ambayo iliitoa Senegal katika hatua ya 16 bora.

Deschamps amesema kuwa, timu yake iko shwari kabla ya pambano hilo na imejiimarisha kuelekea hatua za baadaye za mashindano.

Ufaransa itaumana na Uingereza leo Desemba 10, 2022 katika hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) katika Dimba la Al-Bayt lililopo Al Khor, Qatar,

"Tumekuwa na utulivu mkubwa, tumekuwa nao tangu kuanza kwa mashindano," Deschamps alisema. "Ni robo fainali ya Kombe la Dunia. Kwa hiyo, kwetu ni furaha na raha tu."

Ufaransa pia inakabiliwa na uwezekano wa kuwapoteza wachezaji wake wawili wenye ushawishi mkubwa huku Jules Kounde na Aurelien Tchouameni wakipewa nafasi hasi.

"Wanajua hilo," Deschamps alisema. "Lazima wawe wasikivu, lakini lengo liko wazi na liko pamoja. Tishio lipo, lakini hilo si jambo la maana."

Kasi

Ufaransa pia ina kasi kubwa katika timu yao, huku nyota wa sasa wa michuano hiyo Kylian Mbappe akiongoza kundi hilo.

Hata hivyo, Deschamps amesema, Uingereza inaweza kutumia kasi kujinufaisha licha ya kwamba hakuna upande unaotegemea kasi pekee.

"Unapoenda kwa kasi, mpinzani ana muda mchache wa kujipanga, lakini kasi haifungi mabao," Deschamps alisema.

"Lazima ufanye mabadiliko ya haraka, lakini kwa ubora. Sio bahati mbaya kwamba Uingereza wako hapa. Kasi itakuwa moja ya ufunguo.

"Hii haitoshi kila wakati kufunga. Ni kweli kwamba Waingereza wamefunga mabao mengi katika mabadiliko. Lakini huu sio ubora wao pekee".

Udhaifu

Deschamps pia anaamini kwamba, hakuna udhaifu dhahiri katika upande wa kikosi cha Uingereza. "Kila timu ina mambo ambayo inafanya vizuri sana, tena tofauti na wengine, jambo ambalo mimi na wenzangu tunapaswa kufanyia kazi, ni kujua wapi wana madhaifu zaidi. Si rahisi kujua ni wapi tunaweza kuwapigia".

Bila shaka Mbappe atakuwa mmoja wa wachezaji wa kuangaliwa huku mshambuliaji huyo wa Ufaransa hadi sasa akifunga mabao matano na kusaidia mengine mawili.

"Nadhani Uingereza watakuwa na mpango wao dhidi yake, na Kylian atalazimika kufanya maamuzi," Deschamps alisema.

"Ni jambo la kawaida kuwa na umakini maalum kwa Mbappe, lakini pia ana uwezo huo wa kuamua. Ni mchezaji muhimu na ni wazi wapinzani huwa wanapanga mpango wa kumzuia, lakini Kylian atabaki kuwa Kylian siku zote, atakuwa na uwezo huo, kutafuta suluhu,"amefafanua Kocha huyo wa Ufaransa.(Marca)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news