Korea Kusini yatinga hatua ya 16 bora kwa bao la lala salama

NA DIRAMAKINI

KOREA Kusini imefunga bao la dakika za lala salama na kuishinda Ureno 2-1, hivyo kufuzu kwa hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Shangwe. (Picha na AP).

Hwang Hee-chan aliyetokea benchi alifunga bao la ushindi katika dakika za majeruhi na kuiokoa Korea Kusini kutoka ukingoni mwa michuano ya Kombe la Dunia.

Mshambuliaji huyo wa Wolverhampton Wanderers alizifumania nyavu Desemba 2, 2022 kwa bao la ushindi dakika ya 91 kwenye Uwanja wa Education City nchini Qatar.

Bao ambalo lilisababisha shangwe na taharuki za ajabu kutoka kwa mashabiki wa Jamhuri ya Korea Kusini ambao walitamani kwa hamu kusonga mbele, lakini dakika tisini za awali wawili hao walikuwa suluhu ya moja kwa moja.

Talisman Son Heung-min, ambaye alitengeneza nafasi hiyo ya ushindi, alianguka chini na kulala chali kwenye uwanja wakati wa filimbi ya mwisho ambapo alionekana akitokwa na machozi.

Baadaye wachezaji wa Korea Kusini walisimama kwenye mduara uwanjani huku wakitazama mechi ya Ghana na Uruguay kwa kutumia simu ya mkononi wakisubiri nafasi yao ya kutinga hatua ya 16 bora kuthibitishwa.

Ureno ambao walikuwa wamebadilika sana walikuwa wamepata bao la kuongoza dakika ya tano kupitia kwa Ricardo Horta, lakini Wakorea, ambao walilazimika kushinda ili kupata nafasi yoyote ya kusalia katika michuano hiyo, walifunga dakika ya 27 kupitia kwa Kim Young-gwon.

Nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo alicheza sehemu ya bao la kusawazisha la Korea Kusini, akipiga kona na mpira kumgonga Kim.

Wakorea Kusini hawakuwa tu wakiwinda ushindi ulioonekana kutowezekana dhidi ya timu ya namba tisa ya Dunia inayoongozwa na Cristiano Ronaldo, lakini pia walilazimika kutegemea matokeo ya mechi nyingine ya Kundi H kati ya Uruguay na Ghana.

Ushindi huo wa dakika za lala salama uliipeleka Korea Kusini hadi nafasi ya pili kwenye msimamo nyuma ya Ureno, ikiwa na alama nne sawa na Uruguay, lakini walikuwa na faida ya kufunga mabao zaidi wakati wa hatua ya makundi baada ya timu hiyo ya Amerika Kusini kushindwa kushinda kwa goli moja katika Uwanja wa Al Janoub.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news