Mama Mariam Mwinyi azindua na kushiriki matembezi ya kilomita tano

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mhe.Mama Mariam Mwinyi (katikati) akishiriki katika matembezi ya kilomita tano yaliyotayarishwa na Taasisi ya Smile for Community chini ya Mkurugenzi Mtendaji,Flora Njelekela (wa tatu kushoto) pamoja na viongozi mbalimbali na wananchi kuanzia Ngome Konge,Mlandege hadi Viwanja vya Maisara jijini Zanzibar leo Desemba 3, 2022. Mke wa Rais wa Zanzibar pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mhe.Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mhe.Riziki Pembe Juma (kulia) alipowasili katika Bustani ya Forodhani kwa ajili ya kuzindua mbio za kilomita tano na 10 wakiwemo na watu wenye ulemavu, matembezi yaliyotayarishwa na Taasisi ya Smile for Community kuanzia Ngome Konge,Mlandege hadi Viwanja vya Maisara jijini Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mhe.Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Katibu Mkuu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ndg,Abeda Rashid Abdalla (kulia) alipowasili katika Bustani ya Forodhani kwa ajili ya kuzindua mbio za kilomita tano, na 10 wakiwemo watu wenye ulemavu, matembezi yaliyotayarishwa na Taasisi ya Smile for Community kuanzia Ngome Konge,Mlandege hadi Viwanja vya Maisara jijini Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mhe.Mama Mariam Mwinyi akifyatua bastola kama ishara ya kuzindua mbio za kilomita kumi sambamba na kilomita tano zilizojumuisha watu wenye ulemavu, matembezi yaliyotayarishwa na Taasisi ya Smile for Community kuanzia Ngome Konge,Mlandege hadi Viwanja vya Maisara jijini Zanzibar.
Wanariadha wa mbio za kilomita tano sambamba na matembezi wakiwemo na watu wenye ulemavu tafauti wakijitayarisha kabla mbio hizo kuzinduliwa leo Desemba 3, 2022 na Mke wa Rais wa Zanzibar pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mhe.Mama Mariam Mwinyi,ambapo taasisi ya Smile for Community imeandaa matembezi hayo kuanzia Ngome Konge,Mlandege hadi Viwanja vya Maisara jijini Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe.Mama Mariam Mwinyi (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mhe.Riziki Pembe Juma (kulia) mara baada ya kumalizika kwa matembezi ya kilomita tano yaliyofanyika leo sambamba na mbio za kilomita tano, na kumi katika hafla iliyotayarishwa na Taasisi ya Smile for Community kuanzia Ngome Konge,Mlandege hadi Viwanja vya Maisara jijini Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe.Mama Mariam Mwinyi (kushoto) akivalishwa nishani na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Smile for Community, Ndg. Flora Njelekela mara baada ya kumalizika kwa matembezi kilomita tano,mbio za kilomita tano na kumi yaliyotayarishwa na Taasisi ya Smile for Community kuanzia Ngome Konge,Mlandege hadi Viwanja vya Maisara jijini Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news