MSIPEPERUSHWE NA MIKUMBO

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wameambiwa kuwa wajifunze namna Yesu alivyomsifu Yohane Mbatizaji kuwa mtu asiyepeperushwa kwa mikumbo mbalimbali ya hewa, maana yake Yohane alikuwa mtu wa misimamo kwa kutimiza ujumbe kwa uaminifu kabisa.

Hayo yamesemwa katika maneno ya utangulizi ya maombi ya misa ya Jumapili ya tatu ya majilio ya Desemba 11, 2022 katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Parokia ya Chamwino Ikulu, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma na Padri Paul Mapalala.

Msomaji wa maombi hayo alimalizia maombi ya misa hiyo yaliyoombea haya, “Uwaongoze raia nchini mwetu wawachague wajumbe wa Bunge bora watakaotunga sheria zinazozingatia haki na amani, ee Bwana.”

Awali kabla ya maombi haya Padri Mapalala alitoa mahubiri ya misa hii akisema wazi kuwa Jumapili hii ni dominika ya furaha ambapo masomo yote yanazungumzia furaha ya kumpata Kristo miongoni mwetu.

“Sasa hivi kila aliyesali leo anafuraha kwa sababu ana imani ya kumpata Kristo na kuwa mwakilishi wake katika mazingira yake popote pale anapoishi; kazini kwako, katika familia, katika jumuiya na kazi yoyote ile unayoifanya. Wewe ndiye Yohane Mbatizaji na wewe ndiye mtangazaji wa Kristo.”

Katika misa hii mwandishi wa ripoti hii alibaini kuwa wakati wa kutakiana amani muumini mmoja badala ya kuinamisha kichwa chini upande alipo muumini mwezake yeye alitoa mkono ambapo kabla ya kuibuka kwa ugonjwa wa UVIKO-19 huo ndiyo ulikuwa utaratibu katika misa na ibada za Kanisa Katoliki.

Mwandishi wa ripoti hii taswira hii ilimpa picha namna majanga mbalimbali yanavyoweza kuyabadilisha maisha ya mwanadamu.

Mpaka misa hii ya kwanza ya Jumapili ya tatu ya majilio inamalizika hali ya hewa ya eneo la Chamwino Ikulu bado imekuwa ya jua kali, lakini wakulima bado hawajakata tamaa wameendelea na kuzifukia mbegu ardhini kusubiri mvua za masika ambazo kwa hakika bado hazijaanza kunyesha katika eneo hili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news