Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi mbalimbali

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Desemba 16, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said ambapo uteuzi umeanza tarehe hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Afua Khalfan Mohamed kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Karume, Sayansi na Teknolojia Zanzibar.

Pia, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Abdulla Saleh Omar kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ajira katika Ofisi ya Rais, kazi, Uchumi na Uwekezaji.

Ndugu Omar kabla ya uteuzi huo, kwa mujibu wa taarifa ya Mhandisi Zena alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee.

Desemba 14, 2022 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Mwinyi alifanya uteuzi mwingine kwa viongozi mbalimbali ambapo uteuzi huo ulianza tarehe hiyo.

Miongoni mwa walioteuliwa katika Tume ya Mipango ni Dkt.Ameir Haji Sheha kuwa Kamishna wa Idara ya Ukuzaji Uchumi.

Dkt.Ameir amewahi kuwa Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi katia Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Desemba 14, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alimteua Mohamed Masoud Salim kuwa Kamishna wa Idara ya Mipango ya Kitaifa, Maendeleo ya Kisekta na Kupunguza Umaskini.

Ndugu Mohamed kabla ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alikuwa Meneja wa Pensheni katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Pia Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alimteua Dkt.Rukkaya Wakif Muhammed kuwa Kamishna wa Idara ya Mipango na Maendeleo ya Watendakazi.

Dkt.Rukkaya kabla ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alikuwa Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU).

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amefanya uteuzi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Mhandisi Zena, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alimteua Zainab Khamis Kibwana kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Ndugu Zainab kabla ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alikuwa Mwanasheria katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.

Kwa upande wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi alimteua Zahor Salum Elkhrous kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uratibu wa Uchumi wa Buluu Zanzibar.

Ndugu Zahor Salum Elkhrous aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu Tanzania.

Mbali na hayo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alifanya uteuzi katika Wizara ya Maendeleo ya Jinsia , Wazee na Watoto.

Walioteuliwa ni Bihindi Nassor Khatib kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti. Ndugu Bihindi aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA).

Pia kwa mujibu wa taarifa ya Mhandisi Zena, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alimteua Sitti Abass Ali kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia na Maendeleo ya Jamii.
 
Kabla ya uteuzi wa ndugu Sitti alikuwa Kamishna wa Idara ya Mipango ya Kitaifa, Maendeleo ya Kisekta na Kupunguza Umasikini.

Aidha, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Hassan Ibarahim Suleiman kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee. Ndugu Hassan kabla ya uteuzi huo alikuwa Mwalimu wa Skuli ya Sekondari ya Haile Salassie.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news