Rais Dkt.Samia afanya uteuzi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa makatibu wakuu wawili wa wizara.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Desemba 14, 2022 na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu,Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais, Dkt. Samia amemteua Dkt. Hashil Twaib Abdallah kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Abdallah alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara (Uwekezaji).

Aidha, Rais Dkt. Samia amemteua, Kaspar Kaspar Mmuya kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kabla ya uteuzi huo,Mmuya alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huu ni kuanzia Desemba 9, 2022.

Post a Comment

0 Comments