Serikali yaendelea kuimarisha uratibu katika utekelezaji wa dhana ya Afya Moja

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imeendelea kuimarisha uratibu katika utekelezaji wa dhana ya Afya Moja kwa kushirikiana na wadau wote wa Afya na wadau wa maendeleo kwa ujumla ili kulinda afya ya jamii na kuifanya Tanzania kuendelea kuwa mahala salama wakati wote dhidi ya matishio mbalimbali ya kiafya.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Bw. Prudence Constantine akifungua Mkutano wa Maafisa Viungo wa Afya Moja kwa ajili ya Tathimini ya Utekelezaji wa Shughuli za Afya Moja kwa mwaka 2022 uliofanyika tarehe 13 Desemba, 2022 katika Ukumbi wa mikutano hoteli ya Edema Mkoani Morogoro.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Bw. Prudence Constantine wakati akifungua Mkutano wa Maafisa Viungo wa Afya Moja walipokutana kwa siku mbili kwa lengo la Kufanya Tathimini ya Utekelezaji wa Shughuli za Afya Moja kwa mwaka 2022 tarehe 13 Disemba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Edema Mkoani Morogoro.

Alisema kuwa, Serikali imeendelea kuimarisha uratibu katika utekelezaji wa shughuli za Afya Moja kwa kutekeleza masuala kadhaa ikiwemo kufuta Dawati la Afya Moja na kuanzisha Sehemu ya Afya Moja (One Health Section) katika Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, pamoja na kuhuisha Mpango Mkakati wa Taifa wa Afya Moja 2015 – 2020 kwa kushirikiana na wadau.

Akieleza kuhusu dhana ya Afya Moja alisema,inawakutanisha wataalam na wadau kutoka sekta mbalimbali, hususani sekta za Afya ya Binadamu, Mifugo, Wanyama pori, Mazingira na Kilimo katika kutekeleza Agenda ya Usalama wa Afya Duniani.
Mratibu wa Mradi kutoka RBA Initiative (Roll Back Antimicrobial Resistance Initiative Bw. Michael Mosha akiwasilisha mada wakati wa mkutano wadau wa Afya.

“Dhana hii ina manufaa makubwa hasa katika nchi zinazoendelea kwa kuwa inatumia rasilimali chache zilizopo kwa ufanisi weye matokeo chanya,” alisisitiza.

Alifafanua kuwa ushirikiano baina ya wataalam na sekta za Afya ya Binadamu, Wanyama, Kilimo na Mazingira (Afya Moja) hivi sasa ni agenda ya dunia ambapo imedhihirika kupunguza gharama katika kushughulikia tishio la milipuko ya magonjwa yanayotokana na vimelea vinavyoweza kuenea kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu katika mazingira mbalimbali.
Mtaalam wa Epidemiolojia kutoka Shirikia la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt. Niwael Mtui akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.

Pia ushirikiano baina ya sekta zote za Afya Moja unategemea sana maafisa viungo waliopo katika sekta hizo ili kusaidia utendaji kazi wa Sehemu ya Afya Moja.
Mtaalam Mshauri wa Afya Moja kutoka Taasisi ya RBA Initiative (Roll Back Antimicrobial Resistance Initiative), Bw. Harrison Chinyuka akiongoza mkutano wa wadau wa Afya Moja.

“Tuendelee kutekeleza majukumu yetu ipasavyo kama maaafisa viungo ili sekta zetu zishiriki kikamilifu katika utekelezaji wa dhana ya afya moja na kuleta matokeo chanya katika kupanua na kuimarisha ushirikiano baina ya sekta/taaluma mbalimbali katika hatua zote za kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na milipuko ya magonjwa na hatari nyingine za afya zinazohitaji ushiriki wa sekta zaidi ya moja na taaluma mbalimbali,”alieleza Prudence.
Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt. Andrew Yona Kitua akizungmza wakati wa mkutano wa wadau wa Afya Moja.

Aidha ushirikiano huu pamoja na wadau wengine ikiwemo jamii, kimsingi unaongozwa na sekta/wizara za msingi (lead Ministries) ambazo ni Afya ya Binadamu, Wanyama (Mifugo na Wanyama Pori), Mazingira na Kilimo katika ngazi zote.

“Ni imani yangu kuwa, mnatambua umuhimu wa kuimarisha na kuboresha utekelezaji wa dhana ya Afya Moja nchini na hatimaye kulinda na kuboresha afya ya binadamu, wanyama na uhifadhi wa mazingira pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchini,”alisema Prudence.
Mshauri Elekezi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Bi.Peragia Muchuruza akichagia hoja wakati wa mkutano huo.
Mratibu wa Afya Moja Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt.Baltazar Leba akichangia jambo wakati wa mkutano huo.

AWALI

Afya Moja ni dhana ya kimataifa iliyoridhiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), shirika linaloshughulika na Afya ya Wanyama (OIE), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Programu ya Kimataifa ya Mazingira (UNEP) kupitia “Global Health Security Agenda” (GHSA) na wadau wengine wa Afya duniani kote.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Bw. Prudence Constantine (Katikati mwenye Suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa Maafisa Viungo wa Afya Moja kwa ajili ya Tathimini ya Utekelezaji wa Shughuli za Afya Moja kwa mwaka 2022 uliofanyika tarehe 13 Desemba, 2022 katika Ukumbi wa mikutano hoteli ya Edema Mkoani Morogoro.

Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika linaloshughulika na Afya ya Wanyama (OIE) na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) yamekuwa yakishirikiana duniani kote na kutoa wito kwa wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu, Wanyama na Mazingira kuongeza na kuimarisha ushirikiano na mawasiliano.

Lengo ni kuboresha ufanisi katika kukabiliana na tishio la magonjwa ya kuambukiza yanayoenea kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu na yanayovuka mipaka, tatizo la usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, usalama wa chakula na lishe, afya ya mazingira, usalama na ulinzi wa vimelea hatarishi vya magonjwa na changamoto zingine zinazokabili afya ya jamii zinazohitaji nguvu ya pamoja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news