Serikali yatoa milioni 50/- kumalizia ujenzi wa Zahanati Mtumile

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeahidi kutoa fedha ili kumalizia ujenzi wa boma la zahanati ya Mtumile baada ya nguvu kazi za wananchi kufikia hatua ya kuezeka bati.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu (Mb), Mhe. George Simbachawene akikagua boma la zahanati ya Mtumile lillilopo kata ya Kibakwe.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu (Mb), Mhe. George Simbachawene katika Mkutano wa hadhara alioufanya katika Kijiji cha Mtumile jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
“Serikali itatoa shilingi millioni 50 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa boma la zahanati hiyo pamoja na kuanza ujenzi wa nyumba mbili za watumishi kwa kutumia fedha hizo.

"Nguvu zenu mlizojitolea na nguvu zangu nilizojitolea haziwezi kwenda bure, Serikali ya Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imesikia kilio chetu."
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akikagua ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Mtumile,

Amefafanua katika mkutano wa Mkuu wa 10 wa Chama uliopita Mhe. Rais alielekeza viongozi kuhakikisha tunachapa kazi na kutenda haki kwa wananchi tunaowaongoza.

“Niwaombe viongozi simamieni watu wafanye kazi, kazi ya serikali ni kuweka huduma za msingi za kijamii ambazo zipo kwa kiasi kikubwa,”amesema Waziri Simbachawene.

Akitoa salamu za kumkaribisha Waziri, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. Richad Maponda amesema kuna kazi nzuri zimefanywa katika jimbo la Kibakwe ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, elimu afya na umeme.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu (Mb), Mhe. George Simbachawene akizungumza jambo na Diwani wa Kata ya Kibakwe Mhe. David Chisanza.

“Tunapaswa kuungana na kiongozi wetu: kwa kumuamini katika kazi zilizotangulia kufanyika, maendeleo ni kupanga na kuchagua. huwezi kuyafanya yote kwa wakati mmoja, kuna mambo yatatangulia na mengine yatabaki.”

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtumile, Bw.Tito Mduwile ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa fedha ilizopatia serikali ya kijiji ambazo zimesaidia kuimarisha miundombinu ya elimu na afya.

“Kiasi cha milioni 25 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa Shule ya Msingi Mtumile, na kiasi kingine cha fedha za madawati zilizotolewa na wadau wa elimu ikiwa ni pamoja na fedha kutoka mfuko wa jimbo ambazo zimetumika kupauwa zahanati ya Mtumile.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news