TANZANIA,OMAN ZAAINISHA MAENEO YA KUSHIRIKIANA

NA MWANDISHI WETU

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania na Oman zimedhamiria kuchukua jitihada za makusudi kuimarisha ushikiano wa kiuchumi baina ya nchi hizo zenye uhusiano madhubuti wa kihistoria.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena L. Tax (Mb) na mwenyeji wake, Mhe. Sayyid Badr Al Busaidi wakiwa katika mazungumzo pembezoni mwa Mkutano wa Pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Oman uliohitimishwa jijini Muscat tarehe 11 Desemba 2022.

Hayo yamebainishwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi hizo, Mhe. Dkt. Stergomena L.Tax (Mb) na mwenyeji wake, Mhe. Sayyid Badr Al Busaidi walipokutana pembezoni mwa Mkutano wa Pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Oman uliohitimishwa jijini Muscat tarehe 11 Desemba 2022.

Katika hotuba zao za kufunga Mkutano wa Pili wa JPC, Viongozi hao walieleza kuwa nchi zao zimekubaliana kuanzisha Kamati ya Pamoja ya Kufuatilia Utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano huo ili kuwa na tija kwa pande zote mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena L. Tax (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mhe. Sayyid Badr Al Busaidi waliipokutana pembezoni mwa Mkutano wa Pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Oman uliohitimishwa jijini Muscat tarehe 11 Desemba 2022.
Meza Kuu wakati wa Mkutano wa Pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Oman uliohitimishwa jijini Muscat tarehe 11 Desemba 2022.

Kamati hiyo pamoja na mambo meningine, itahkikisha rasimu zote za mikataba na makubaliano zinakamilika na kutiwa saini ili kujenga mazingira ya kisheria ya kuimarisha uhusiano wa kindugu uliopo baina ya Tanzania na Oman.

Maeneo yaliyojadiliwa na ujumbe wa nchi hizo na kuwekewa mikakati ya utekelezaji ni pamoja na kilimo, elimu, nishati, biashara, uwekezaji, mawasiliano, mifugo na usafirishaji. Maeneo mengine ni uvuvi, utalii, michezo, utamaduni, madini,uhamiaji, fedha na udhibiti wa majanga ya moto.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena L. Tax (Mb) akibadilishana nyaraka zenye masuala yaliyoafikiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mhe. Sayyid Badr Al Busaidi wakati wa Mkutano wa Pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Oman uliohitimishwa jijini Muscat tarehe 11 Desemba 2022.

Mkutano wa JPC kati ya Tanzania na Oman ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena L. Tax; Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato; Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu; Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab; Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Ndugu Kheri Mahimbali; na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar, Ndugu Mwanahamisi Adam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news