Wanafunzi washauriwa kufika kusaini fedha zao kabla ya kurejeshwa HESLB

NA DIRAMAKINI

KAMISHNA wa Mikopo Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Emanuel Martine amewahimiza wanafunzi wote vyuoni wahakikishe wanasaini fedha zao kabla ya siku 30 kumalizika ili zisirudishwe Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Martine amesema,Serikali inatoa fedha,hivyo wanafunzi wanapaswa kuzisaini fedha hizo kwa wakati sahihi bila kupoteza muda vyuoni.

"Fedha zinakaa chuoni kwa siku 30 tu, baada ya hapo zinarudishwa HESLB, TAHLISO tunaomba wanafunzi vyuoni wajitahidi na wajitokeze kusaini fedha hizo kwa wakati sahihi,"amefafanua Martine.

Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa leo Desemba 4, 2022 amefafanua kuwa, wanafunzi ambao mikopo yao ipo vyuo vingine wahakikishe taarifa zao wanazipeleka kwa LOAN OFFICERS wao ili waweze kuanza michakato ya kuzifuatilia kwenye vyuo zilipo ili baada ya retirement fedha hizo ziweze kuelekezwa kwa wahusika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news