WAZIRI MKUU AAGIZA WAKUU WA WILAYA KUKUTANA NA WAFUGAJI

*Pia asisitiza vikao vya pamoja vya maridhiano ya wakulima na wafugaji

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza Wakuu wa Wilaya kuitisha vikao na wafugaji ili kujadiliana na kuweka namna bora ya kufanya shughuli za ufugaji ikiwa ni pamoja na kutambua mifugo yote iliyoko ndani ya Wilaya husika na kuweka zuio la mifugo mingine kuingizwa katika wilaya zao.
Mheshimiwa Majaliwa pia ameagiza viongozi katika mikoa na wilaya kuweka mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye maeneo yote yenye wafugaji na wakulima ambapo pia kuna vyanzo vya maji.

Amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka kuona uharibu wa vyanzo vyote vya maji vinadhibitiwa kwa kuwekewa mpango mkakati utakaowezesha kuyatunza maeneo hayo dhidi ya uharibifu wa aina yeyote.
Amesema hayo Disemba 24, 2022 katika kikao cha pamoja na Mawaziri wa Kisekta, Makatibu na Naibu Makatibu wakuu kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na Wilaya za Morogoro wadau na wasimamizi wa masuala ya ardhi na mifugo ili kutatua, changamoto za usimamizi wa masuala ya ardhi ndani ya Mkoa huo.

Kikao hicho kimefuatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheahimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa Desemba 22, 2022 Wakati akifunga njia ya kuchepusha maji na kuanza ujazaji maji kwenye bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP).

“Agizo la Mheshimiwa Rais ni lazima litekelezwe kwa sisi wasaidizi kutimiza wajibu wetu na kuweka mikakati ya kutekeleza agizo hilo kwa ufanisi.Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa amewataka wakuu wa Wilaya kuunda kamati za maridhiano baina ya wafugaji na wakulima, ili kutengeneza umoja kati ya makundi hayo mawili “Wafugaji washirikishwe kuandaa miundombinu ambayo wanyama wao wataitumia kupata malisho, maji pamoja na majosho”

Aidha, Mheshimiwa Waziri Mkuu amekemea vitendo vya rushwa kuanzia kwenye ngazi ya viongozi wa Serikali za vijiji “unakuta kiongozi wa kijiji anaruhusu wafugaji kutoka maeneo mbalimbali kwasababu tu amepewa rushwa na anasahau athari ambazo wanazipata wanavijiji wao”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news