BAVICHA watoa neno kuhusu vigezo vya ajira

NA DIRAMAKINI

MWENYEKITI wa Baraza la Vijana Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), John Pambalu ameiomba Serikali kulegeza kigezo cha uzoefu wa kazi kama mojawapo ya sharti la ajira kwa vijana.

Pambalu amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho.

“Ipo haja serikali kulegeza masharti ya ajira kwa vijana kwa kuwa kwa sasa vijana wengi wanakosa ajira kwa kigezo cha uzoefu wa kazi na badala yake wapewe kazi chini ya usimamizi wa kipindi cha miezi kadhaa au miaka kadhaa,”amesema.

Pambalu amesema ipo haja uchunguzi ufanyike kwa kina kuhusu walengwa na wanaopata mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri kwa vijana kwa kile alichodai kuwa mikopo hiyo hutolewa kwa upendeleo.

Ameiomba serikali itoe masharti nafuu kupitia taasisi za kifedha hususani zile za serikali ili kijana anapohitimu masomo ajiajiri na kufanya biashara.

Akijibu maswali ya waandishi kuhusu kufanya siasa za kistaarabu na si za matusi amesema swali hilo viulizwe vyama ambavyo havina sera na ilani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news