Halmashauri zakusanya bilioni 485.42/-

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Angellah Kairuki amesema kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba 2022 kwa mwaka wa fedha 2022/23 halmashauri zimekusanya jumla ya shilingi bilioni 485.42 sawa na asilimia 48 ya lengo la mwaka na asilimia 96 ya lengo la nusu mwaka.
Mheshimiwa Kairuki ameeleza hayo Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani katika mamlaka za Serikali za mitaa kwa kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2022/23 kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.

Amesema, katika makusanyo hayo, mapato yasiyolindwa ni shilingi bilioni 396.67 na mapato lindwa ni shilingi bilioni 88.73.
“Katika mwaka wa fedha wa 2022/23, halmashauri ziliidhinishiwa kukusanya shilingi trilioni 1.02 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani,"amesema.

Waziri Kairuki amesema, makisio ya mapato ya ndani yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 863.90 mwaka 2021/22 hadi shilingi trilioni 1.012 mwaka 2022/23 sawa na ongezeko la asilimia 17 ambapo ni ongezeko la shilingi bilioni 148.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news