RC Makalla apiga marufuku biashara barabara za mwendokasi

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla leo amefanya zoezi la usafi Wilaya ya Temeke eneo la Mbagala, ambapo amepiga marufuku ufanyaji biashara kwenye ujenzi wa barabara ya mwendokasi na maeneo yaliyokatazwa.

RC Makalla ametumia zoezi hilo kuwakumbusha wananchi na viongozi kuanzia ngazi ya mtaa hadi wilaya kuhakikisha wanasimamia usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Aidha, RC Makalla amewaelekeza wakurugenzi kusimamia wakandarasi kuondosha taka kwa wakati na wakandarasi watakaoonyesha kulegalega wasipatiwe mkataba.

Pamoja na hayo RC Makalla amewapongeza wananchi kwa mwamko mkubwa wa kufanya usafi jambo lililopelekea Jiji la Dar es Salaam kushika nafasi ya sita kwa usafi barani Afrika na kuondosha magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindipindu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news