Kocha Mkuu wa Simba SC asema hawana shughuli ndogo, kazi imeanza rasmi

NA DIRAMAKINI

KOCHA Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera (Robertinho) amesema, ushindi wa mabao 3-2 waliopata Januari 18, 2023 dhidi ya Mbeya City ni jambo la kwanza alilokuwa anahitaji na limemfanya afurahi.

Robertinho amesema amefurahishwa na wachezaji walivyocheza kitimu licha ya kuwa amekaa nao kwa muda mfupi.

“Ilihitajika ushindi bila kujali tumechezaje, tupo kwenye mbio za ubingwa tunapaswa kushinda kila mchezo hasa tukiwa nyumbani.

“Ndiyo kwanza nina siku nane tangu nilipoanza kazi. Simba ni timu kubwa na malengo yake ni makubwa pia kama nilivyo mimi.

“Jambo jingine lililonifurahisha ni jinsi tulivyocheza, wachezaji walicheza kitimu ingawa kulikuwa na makosa kadhaa ambayo tunapaswa kuyaondoa.Nimeanza kupata mwanga wa kikosi ambavyo kinapaswa kiwe,”amesema Robertinho

Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Saido Ntibazonkiza aliwapatia bao la kwanza dakika ya 10 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa fundi Clatous Chama aliyepokea mpira wa Bocco.

Bao hilo lilidumu kwa dakika mbili tu kwani Mbeya City walisawazisha dakika ya 12 kupitia kwa Richardson Ng’ondya aliyepokea pasi ya Salim Kihimbwa.

Ntibazonkiza alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 48 baada ya mlinzi Mohamed Hussein kuchezewa madhambi ndani ya 18 na Ng’ondya.

Pape Sakho alitupatia bao la tatu dakika ya 55 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea pasi ya Ntibazonkiza aliyempora mpira Ng’ondya.

Mbeya City ililalazimika kucheza wakiwa pungufu kwa dakika 25 za mwisho baada ya mlinzi wa kati Samson Madeleke kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea madhambi Sakho dakika ya 65.

Aidha, Mbeya City walipata bao la pili dakika ya 78 kupitia kwa mlinzi Juma Shemvuni kwa mpira mrefu katikati ya uwanja baada ya mlinda mlango Aishi Manula kusogea mbele na kuliacha lango.

Kikosi cha Simba kilikuwa namna hii, X1: Manula, Kapombe, Zimbwe Jr, Onyango, Ouattara, Kanoute, Kyombo (Erasto Nyoni 91′), Mzamiru, Bocco (Kibu Denis 33′) Ntibazonkiza, Chama (Pape Sakho 33′)

Wachezaji wa Akiba ambao hawakutumika: Beno Kakolanya, Gadiel Michael, Nassor Kapama, Jimmyson Mwanuke.

Walionyeshwa kadi: Kanoute 43′ Mzamiru 57′ Onyango 67′ Manula 79′ Sakho 94′

X1: Kanyonga, Kunambi, Mwankemwa, Madeleke, Shemvuni, Ndunguli (Abdulrazak Mohamed 73′) Ng’ondya (Eliud Ambokile 63′) Hassan Nassor, Tariq, Awadh Juma (Sixtus Sabilo 62), Kihimbwa (Jamal Dullaz 84′)

Wachezaji wa Akiba ambao hawakutumika: Haroun Mandanda, Eradius Salvatory, Baliko Anyimke, Gaspar Mwaipasi, Baraka Mwalubunju.

Walionyeshwa kadi: Hassan Nassor 46′ Madeleke 52′ 66′ (nyekundu) Tariq Seif 67′ Kenneth Kunambi 71′.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news