KVZ yatwaa Kombe la Netiboli Mapinduzi Cup 2023

NA DIRAMAKINI

TIMU ya Netiboli ya Kikosi cha KVZ imeibuka kidedea katika Fainali za Mashindano ya Netiboli Mapinduzi Cup 2023 ulichozwa katika Viwanja vya Gymkhana,Unguja jijini Zanzibar.
Mchezo huo wa fainali ulihusisha timu za Wanawake kutoka Vikosi vya KVZ na Zimamoto, ambapo KVZ imefanikiwa kuichapa Zimamoto magoli 50 kwa 39.

Mpaka kufikia mzunguuko wa tatu wa mapumziko katika mchezo huo, KVZ ilionekana kuongoza kwa magoli 37 dhidi ya Zimamoto kwa kuwa na magoli 27.
Akizugumza baada ya kumalizika mchezo huo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Riziki Pembe Juma amewapongeza washindi pamoja na washiriki wote wa mchezo huo wa netiboli kwa kushiriki mchezo huo kwa ushirikiano mzuri pamoja na nidhamu ya hali ya juu.

Amesema, michezo ni afya, michezo pia inajenga ushirikiano na nidhamu, hivyo amewataka kuendeleza ushirikiano huo pamoja na nidhamu katika sehemu nyengine ili kufikia malengo yao.
Aidha, amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi makini wa Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi umeahidi kuweka kipaumbele katika michezo katika bajeti yake ya 2023-2024, kwa kuendelea kujenga viwanja vya michezo vya kisasa kwa lengo la kuimarisha michezo hapa nchini.

Hivyo amesema, changamoto yao ya ukosefu wa viwanja vya kisasa anaamini Rais Dkt.Mwinyi ataitatua, na kuwaonba kuwa na uvumilivu katika kufikia malengo hyo.
Pia Mhe.Riziki alitumia fursa hiyo, kuwaomba wakuu wa vikosi hivyo kuangalia uwezekano wa kuwapandisha vyeo wachezaji wake hasa wanawake, kwani wamekuwa wakiwaletea sifa kubwa vikosi vyao katika michezo.

Naye Katibu wa Chama cha Netiboli Zanzibar (CHANEZA), Said Ali Mansab amesema mashindano hayo kikawaida hufanyika kila mwaka ikiwa lengo ni kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, kuwa ni chachu ya kuinua michezo Zanzibar pamoja na kuinua vipaji vya vijana katika kujipatia ajira kimichezo.

Amesema, mashindano hayo ya Netiboli Mapinduzi Cup, yalianza Januari 4, mwaka 2023 ambapo jumla ya timu saba zilishiriki, ikwemo KVZ, Zimamoto, Bandari, Mafunzo, Afya, Ztalent na timu ya Worious.
Katika mchezo huo wa Fainali, KVZ ilijinyakulia kombe la ushindi, fedha taslimu shilingi milioni moja, pamoja na medali, huku zimamoto iliyoshika nafasi ya pili ilipata medali na fedha taslimu shilingi laki tano na mshindi wa tatu timu ya Bandari ilijinyakulia kombe la nidhamu pamoja na medali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news