Mgunda, Chama wang'ara

NA DIRAMAKINI

KOCHA Juma Mgunda amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara huku Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama akichaguliwa mchezaji bora.

Mgunda aliiwezesha Simba SC kushinda mechi nne na kutoka sare moja katika mwezi huo huku akiwapiku Nasreddine Al Nabi wa Yanga na Hans Van Pluijm wa Singida Big Stars.

Kwa upande wake Chama amekuwa kwenye ubora na takwimu nzuri katika mwezi Desemba akicheza mechi tano sawa na dakika 450 akifunga mabao mawili na asisti tano.

Chama amewapiku Nahodha John Bocco na mshambuliaji Fiston Mayele ambao ameingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Takwimu za Mgunda za Desemba

Coastal Union 0-3 Simba

Geita Gold 0-5 Simba

Kagera Sugar 1-1 Simba

KMC 1-3 Simba

Simba 7-1 Tanzania Prisons

Mgunda ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo pia mwezi Novemba, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news