Mkurugenzi na Mhariri Mtendaji wa DIRAMAKINI, Godfrey Ismaely Nnko atunukiwa tuzo ya Kimataifa

NA DIRAMAKINI

WAKFU wa Chinmaya (Chinmaya Foundation) umemtunuku Mkurugenzi Mtendaji wa Diramakini Business Limited, Bw.Godfrey Ismaely Nnko tuzo ya Kimataifa ya 'Man of the Year 2022' kutokana na mchango chanya alioutoa kupitia DIRAMAKINI kwa kuhabarisha umma kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo jamii, utamaduni, diplomasia, amani, elimu, afya Kitaifa na Kimataifa kupitia chombo hicho cha habari.

Nnko ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa DIRAMAKINI ametajwa kuwa na mchango mkubwa kwa kufanya machaguo sahihi ya taarifa ambazo zimeendelea kuwa shirikishi na jumuishi katika jamii kupitia tovuti hiyo.

"Tumeridhika kukutunuku tuzo hii ya mwaka ya Kimataifa, kutokana na kipaji chako cha kuchakata na kufanya machaguo sahihi ya habari zinazogusa maisha ya watu Kitaifa na Kimataifa.

"Wewe (Godfrey Ismaely Nnko) ni miongoni mwa watunukiwa 13 wanaotunukiwa Tuzo Bora ya Kimataifa ya Mwaka na Wakfu wa Chinmaya 2022 kutoka mataifa mbalimbali Duniani,"amefafanua mwasisi na Mwenyekiti wa wakfu huo,Dkt.Chinmaya Dash.

Wakfu huo ambao umejiimarisha katika kuleta mapatanisho na kuunganisha jamii duniani umetoa tuzo hiyo Januari Mosi, 2023 katika ofisi za makao makuu zilizopo Mtaa wa Dasarathpur, Babalpur ndani ya Wilaya ya Jajpur katika Jimbo la Odisha nchini India.

Aidha, Chinmaya Foundation ilichagua vipaji 13 kutoka nchi 10 zikiwemo India, Nigeria, Nepal, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bangladesh, Afrika Kusini, Syria, Paraguay, Ufilipino na Afghanistan.

Mbali na Godfrey Ismaely Nnko, wengine waliotunukiwa Tuzo Bora ya Kimataifa ya Mwaka na Wakfu wa Chinmaya 2022 ni msanii mwandamizi Shilpi Kesu Das,Mkurugenzi Mtendaji wa Baleswari Kala Kendra of Koshamba Nagar of Balasore nchini India, David Gachuhi,Mkurugenzi Mtendaji wa Daga Finder Enterprises of Kenya, Dkt. Chidi Ijeoma, mkufunzi wa lugha ya Kifaransa Imo State University of Nigeria.

Cyriacus Kaduru,The Senior Social Worker of Nigeria, Sheila Mhlongo, The Publishing Editor of KZN - Namuhla Community Newspaper of Durban- KZN of South Africa, Hajji Kaysh Chy, The Senior Journalists & co.ordinator in sylhet Division of Ahrc Shundorbon Quriar service gualabazar osmani nagar sylhet of Bangladesh, Rameshwar Yadav, The Senior Educationalist & Writer Nepal,

Anas, The Senior Educationalist in Arabic Language of Syria, Severiano Esquivel Gavilán, The Veteran Social Worker, Paraguay, Dr. Sayed Naqibullah, The General Medical Practitioner in Curative Medicine of Afghanistan, Dr. Nwankwo Tony Nwaezeigwe, The Senior Research Fellow of Institute of African Studies in the University of Nigeria Nsukka Nigeria(Assessing from Manila, Republic of the Philippines).

Wengine ni Aklnleye-Baba Oluwatoyin Grace, The Chief Executive Officer of Ansha Streetwise Media & Digital Ltd. Publisher in Nigeria.

Dkt.Chinmaya amesema, huo ni mwanzo na wanatarajia kuendelea kuwapa heshima zaidi watu mbalimbali duniani kutokana na mchango wao chanya katika kuhabarisha umma na kuunganisha jamii kupitia taaluma na vipaji vyao.

Akizungumzia tuzo hiyo, Mkurugenzi na Mhariri Mtendaji wa DIRAMAKINI, Bw.Godfrey Ismaely Nnko amesema, hiyo ni heshima kubwa kwake inayotokana na ushirikiano mzuri ambao anaupata kutoka kwa wasomaji mbalimbali ndani na nje ya Tanzania wakiwemo wadau mbalimbali wa habari ambao wamekuwa wakiiunga mkono DIRAMAKINI tangu ianze kutoa huduma zake za habari mwishoni mwa mwaka 2020.

"Heshima hii inatokana na ushirikiano ukiwemo mchango mkubwa ninaoupata kutoka kwa wadau mbalimbali wa habari Tanzania, niwashukuru sana kwa kutupa heshima na hadhi hii, ninaamini huu ni mwanzo wa kuendelea kuwahudumia kupitia Sekta ya Habari.

"Mara zote nimekuwa nikisisitiza kuwa, DIRAMAKINI imejipa jukumu la kuchakata na kuchapisha habari chanya ambazo zinagusa, kubadilisha na kuongeza maarifa kwa kila msomaji wetu ndani na nje ya nchi. 
 
"2023, ninaamini ni mwaka wa kufanya makubwa zaidi, na kwa neema za Mungu ninaamini tutafanya mazuri na makubwa zaidi,"amefafanua Bw.Nnko.

Pia amefafanua moja wapo ya siri ya mafanikio ni pamoja na kufanya kazi kwa saa 24, kwa kujitoa kwa hali na mali bila kuchoka.

"Wakati mwingine huwa inafika muda familia inaniona kwamba ninajali sana kazi zangu, kwa sababu ninatumia muda mfupi kwa ajili ya mapumziko, lakini huwa ninasisitiza kuwa, hakuna maisha rahisi, ili uweze kuzifikia ndoto na malengo yako, lazima upambande, nimekuwa nikipambana, kujitoa kwa hali na mali, bila kujali sipati faida zozote zaidi ya kuelimisha na kutoa maarifa kwa jamii,wengi wanahisi ninapoteza muda, lakini ninaamini kuna siku mafanikio yatakuja, na hii ni ishara njema ya huko tuendako,"amefafanua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news