Mo Dewji:Simba SC siku moja itatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Heshima wa Klabu ya Simba na Mwekezaji Mohamed Dewji (Mo Dewji) amewaeleza wachezaji wa klabi hiyo kuwa, nia yake ni siku moja kuiona wanafanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Mo Dewji ameyasema hayo baada ya kutembelea kambi mjini Dubai ambapo amewaambia wachezaji kila kitu kinawezekana kama watafanya jitihada kwenye mechi zao.

Kabla ya kufika hatua ya kuchukua ubingwa wa Afrika, Mo Dewji amewataka wachezaji wapambane kuhakikisha wanarejesha ubingwa wa Ligi na Kombe la Shirikisho la Azam ambapo msimu uliopita walipoteza.

“Siku zote dhamira yangu ni kuhakikisha tunachukua ubingwa wa Kombe la Afrika na hilo linawezekana kama tukiweka nia.

“Kabla ya yote kwanza tuanze na kurejesha ubingwa wetu wa ligi pamoja na Kombe la FA hilo ndilo kubwa, imani yangu ni kuwa kila kitu kinawezekana kama tukiweka jitihada,” amesema Mo Dewji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news