Simba SC kuchuana na Waarabu, Warusi

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Simba SC imepanga kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya CSKA Moscow inayoshiriki Ligi Kuu nchini Urusi.

CSKA Moscow ambayo mara kadhaa imekuwa ikishiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na michuano ya Ligi ya Europa, itacheza na Simba siku ya Januari 15, 2023 huko Dubai. Hayo ni kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa Januari 10, 2023 na klabu hiyo kuelekea michezo miwili ya kirafiki ya Kimataifa.

Simba inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki ikiwa mazoezini Dubai,Januari 13, 2023 dhidi ya Al Dhafrah ya Dubai.

Kikosi hicho kilisafiri Julai 7, 2023 kuelekea Dubai kikiwa na msafara wa watu 38 kwa ajili ya kambi ya mazoezi ya siku kadhaa kujiandaa na mechi za ligi kuu na mashindano mengine.

Kambi hiyo ni mualiko kutoka kwa Rais wa heshima wa klabu, Mohammed Dewji (Mo) ili kuipa nafasi timu ya kufanya maandalizi ya kujiandaa na michuano ligi ya Mabingwa Afrika.

Kambi hiyo ni maalumu kwa ajili ya maandalizi pamoja na kumpa mwalimu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ nafasi ya kuwafahamu wachezaji wake kwa utulivu.

Akizungumzia kambi hiyo Robertinho alisema ni maamuzi sahihi ambayo yatampa nafasi ya kuangalia kikosi chake kwa mapana na kuanza kupandikiza falsafa zake akishirikiana na makocha wenzake, Juma Mgunda na Selemani Matola.

“Ni uamuzi mzuri kwa uongozi kunipa muda wa kufanya mazoezi na kikosi kwa utulivu ili kuniwezesha kuwajua wachezaji nakuwapa mbinu zangu,”amesema Robertinho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news