Prof.Lipumba asisitiza Tume Huru ya Uchaguzi

NA DIRAMAKINI

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeendelea kusisitiza kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025.

Msisitizo huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa CU,F Prof. Ibrahim Lipumba wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa mikutano ya hadhara ya chama hicho.

Prof. Lipumba amesema tume huru ya uchaguzi itawezesha wananchi kupata viongozi wanaowahitaji.Akizungumzia kuhusu mikutano ya hadhara, amesema wataitumia katika kunadi sera za chama na kuimarisha chama nchi nzima.

Awali akizungumza wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa chama, Mkurugenzi wa Habari CUF Taifa,Mhandisi Mohamad Ngulangwa amesema, wakati huu ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu kufuatia zuio lililowekwa kwa vyama vya siasa kutofanya mikutano ya hadhara katika kipindi cha zaidi ya miaka sita.

Amesema, kipekee anapenda kutoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutengua na kuruhusu mikutano ya hadhara kuanza tena baada ya marufuku iliyokuwepo ya mtangulizi wake Rais Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa miaka zaidi ya sita.

Mhandisi Ngulangwa ameongeza kuwa, pamoja na changamoto ambazo kama taifa walizipitia kufuatia zuio hilo katika kipindi chote cha miaka sita haimaanishi kuwa washindwe kupongeza kwa mazuri yaliyofanyika ikiwa ni pamoja na kukosoa kistaarabu na kushauri inapobidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Ubungo, Bashiru Muya akizungumza katika uzinduzi huo amesema mikutano hiyo ya hadhara itasaidia kujenga vyama vya siasa sambamba na kunadi sera zao kwa wananchi kote nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news