Rais Alhaj Dkt.Mwinyi azindua Masjid Istiqama

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Mfadhili wa Ujenzi wa Masjid Istiqama, Bw.Suleiman Mohamed Yahya baada ya kuwasili na kufungua msikiti huo leo Januari 13, 2023,uliojengwa Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi (wa nne kulia) akifungua pazia kama ishara ya Uzinduzi wa Masjid Istiqama leo,Msikiti uliojengwa Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa nguvu za wananchi na ufadhili wa Bw.Suleiman Mohamed Yahya (wa nne kushoto) katika sherehe iliyofanyika sambamba na sala ya Ijumaa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Haroun Ali Suleiman (kushoto) alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi (katikati waliokaa mbele) kuzungumza na waumini baada ya kiufungua Masjid Istiqama,Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja hafla iliyokwenda sambamba na sala ya Ijumaa leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Bw.Suleiman Mohamed Yahya akiwa Mfadhili wa Ujenzi wa Masjid Istiqama katika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja,ambapo ujenzi wake umefanyika kwa kushirikiana na nguvu za wananchi na mfadhili huyo.
Waumini wa Dini ya Kiislamu walioswali sala ya Ijumaa sambamba na ufunguzi wa Masjid Istiqama,Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake leo mara baada Ufunguzi wa Masjid hiyo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake leo mara baada ya sala ya Ijumaa sambamba na Ufunguzi wa Masjid Istiqama katika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja,ambapo ujenzi wake ulifanyika kwa ufadhili wa Sheikh,Suleiman Mohamed Yahya na nguvu za wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi (katikati) pamoja na viongozi wengine na waumini wakiitikia dua iliyosomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi (kushoto) baada ya hafla ya sala ya Ijumaa sambamba na Ufunguzi wa Masjid Istiqama katika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akimpongeza Ramadhan Omar Mcha, wana madrasa waliokuwa wakisoma Qaswida kwa kumsindikiza Rais baada ya hafla ya Ufunguzi wa Masjid Istiqama katika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja, hafla iliyofanyika leo ambapo viongozi mbalimbali na waumini walihudhuria katika sherehe hiyo.

Post a Comment

0 Comments