Elimu ya dini na malezi ni muhimu-Alhaj Abdulla

NA DIRAMAKINI

WAUMINI wa dini ya Kiislamu wametakiwa kutenga muda kwa ajili ya kusoma dini ili kujenga jamii iliyo njema.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo alipojumuika na Waumini wa Msikiti wa Bweleo Wilaya ya Magharibi B katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Amesema, kuwepo kwa matendo maovu katika jamii kunatokana na kukosa elimu ya dini na malezi ambapo jukumu la wazazi kuhimizana kuisoma Dini hatua ambayo jamii itafahamu mambo mema kuyafata na maovu kuyawacha.

Amesema, slimu ni jambo la muhimu ambapo ni vyema kwa waumini kutumia Misikiti kwa kuendeleza masuala ya Dini pamoja na kujadiliana masuala mbali mbali ya kijamii.

Aidha, ameeleza kuwa jamii inaposhikamana na dini inakuwa na nafasi ya kumuabudu Mungu ipasavyo jambo ambalo litasaidia kupata kizazi inayomtambua Mungu na kusimamia maadili mema.

Mhe. Hemed amewasisitiza Waumini hao kuwa na umoja na mshikamano kwa kusaidiana katika masuala mbali mbali ili kuiweka jamii pamoja na yenye upendo.

Akitoa hotuba ya Sala ya Ijumaa Maalim Mussa Ali Kirobo amewataka Waumini hao kusimamia maadili mema hasa kukemea matendo maovu yaliyokithiri na kuwataka kurudi katika mafundisho ya Dini ili kupata kizazi kilicho chema.

Amesema, Zanzibar kwa miaka ya nyuma ilisifika kwa kuwepo wasomi waliobobea katika dini ambao walikuwa tegemezi kwa nchi za Afrika Mashariki na Falme za Kiarabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news