Rais Dkt.Mwinyi:Tutaendelea kushirikiana kuijenga nchi na chama

NA DIRAMAKINI

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaahidi viongozi na wanachama wa Maskani ya Kachorora kushirikiana nao kukijenga chama kiuchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akizungumza na Viongozi na wanachama wa Maskani ya Kachorora CCM walipofika Ikulu jijijini Zanzibar wakiongozwa na Mwenyekiti wa maskani hiyo,Bw.Mohamed Mussa (kulia kwa Rais).
 
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu jijini Zanzibar alipozungumza na viongozi na wanachama wa maskani hiyo waliofika kujitambulisha na kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar.

Amesema, chama kina mkataba na wananchi ambao ni utekelezwaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi na kueleza kuelekea mwaka 2025 watakua na jukumu la kuwaeleza wananchi hao mambo waliyoyafanya kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.

Aidha, Dkt. Mwinyi ameeleza hatua iliyofikiwa ndani ya kipindi cha miaka miwili cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Nane haipo vibaya na matumaini ni makubwa miaka mitano ijayo.

Amewahakikishia wananchi na wanachama cha CCM ndani ya kipindi cha miaka mitano, miradi mikubwa yote iliyoahidiwa itakamilika.

“Tuna makataba na wananchi mkataba ambao ni Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, tunakoelekea mwaka 2025, tutakua na jukumu la kusema yapi katika Ilani ya Uchaguzi tumeyatekeleza, hapo tutakua na haki ya kuomba tena kura,”ameeleza Makamu Mwenyekiti huyo.

Pia amewahakikishia wananchi na wanachama cha CCM ndani ya kipindi cha miaka mitano, miradi mikubwa yote iliyoahidiwa itakamilika.

Akizungumzia masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mfuko wa Uviko-19, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza suala hilo pia limetajwa kwenye Ilani ya uchaguzi na kusema kuwa ingawa sio watu wote watawezeshwa wakati mmoja, lakini alieleza ni suala linalotekelewa kwa awamu na aliwaahidi kila mwananchi atawezeshwa kwa mijibu wa awamu ya fedha zitakavyotoka.

Hivyo, aliwaeleza wanamaskani hao kuisaidia serikali kuwaelimisha wananchi juu ya dhamira yake njema kwao na kuongeza kuwa kiasi cha shilingi bilioni 16 tayari zimetolewa kwa wananchi awamu ya kwanza na shilingi milioni mbili zimeanzwa kurejeshwa ili kufanya mzunguruko wa fedha hizo.

Dkt. Mwinyi aliieleza maskani hiyo kushirikianao nao kwenye ujenzi mzima wa chama na kuwaambia kwamba amedhamiria kukijenga kwa miundombinu imara kuanzia ngazi na shehia hadi taifa kwa kuzimarisha ofisi kwa vifaa vya kisasa pamoja na kuwawezesha watendaji wake.

Aliwaeleza wanamaskani hao dhamira yake ya kukijenga chama kwa vifaa vya kisasa zikiwemo kompyuta, mashine za kudurufu, na vyombo vya usafiri pamoja na kuwezesha maslahi ya watendaji wake badala ya kufanya kazi za chama kwa kujitolea.

Mapema akizungumza kwenye hafla hiyo, Katibu wa tawi hilo Said Shabaan Said, alimueleza Makamu Mwenyekiti huyo kwamba, Chama Cha Mapinduzi daima kinaunga mkono juhudi za Serikali na kueleza kwamba wamekuwa wakifuatilia shughuli za Serikali zinazofanywa na uongozi wa Awamu ya Nane na kuongeza kuwa wanaridhishwa kwa kila hatua ya uongozi huo.

Aidha, wanachama hao walieleza kuiridhishwa na uongozi wa Rais Dkt. Mwinyi wenye kuitekeleza vyema Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi na kueleza kwamba muda wote wako tayari kushirikiana na Serikali pamojana kutekeleza maagizo ya ya chama kwa lengo la kupiga hatua mbele kimaendeleo.

Walieleza imani yao kubwa kwa Makamu Mwenyekiti wa chama, Dkt. Hussein Ali Mwinyi na kumuahidi mafanikio makubwa na ushindi wa kishindo mwaka 2025.

Hata hivyo, walimueleza Rais Dkt.Mwinyi dhamira yao njema ya kuweka vitega uchumi vyao kwenye eneo la maskani yao ambapo walisema wanatarajia ku

Maskani ya Kachorora ilizinduliwa Februari 3 mwaka 2011, wakati wa shamrashamra za maadhimisho ya kilele cha miaka 34 ya Chama Cha Mapinduzi na aliyekua Makamu Mweyekiti kwa wakati huo, Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Sita, Dkt.Amani Abeid Karume.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news