Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua Mwanaisha Juma Fakih kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi na Ukunga katika Wizara ya Afya.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Januari 30, 2023 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said ambapo uteuzi huo umeanza tarehe hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kabla ya Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi kumteua ndugu Mwanaisha alikuwa Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Ukunga katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) katika Kampasi ya Sayansi za Afya Mbweni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news