Simba kuwavaa Mbeya City bila Phiri na Banda leo

NA DIRAMAKINI

KOCHA Msaidizi wa Simba SC, Juma Mgunda amesema maandalizi ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City utakaopigwa saa moja usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, yamekamilika.

Mgunda amesema wachezaji wote wamerejea salama jijini Dar es Salaam kutoka Dubai walikokuwa katika kambi ya siku nane na wako kwenye hali nzuri kupambania alama tatu.

Amesema, wataingia katika mchezo wa leo kwa lengo moja tu la kuhakikisha wanabakisha alama tatu nyumbani.

“Ligi ni ngumu hasa kipindi hiki inapoelekea ukingoni, hivyo tutaingia katika mchezo huo kwa kuchukua tahadhari zote ili tufanikishe lengo letu.

“Tunaiheshimu Mbeya City ni timu nzuri, lakini tupo tayari kupambana kwa ajili ya pointi tatu,” amesema Mgunda.

Katika mchezo wa leo Simba SC itaendelea kukosa huduma ya Moses Phiri na Peter Banda ambao wamerejea mazoezini, lakini hawana utimamu wa asilimia 100.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news