Mo Dewji aahidi kushusha wachezaji wapya, amtaka Robertinho kuchapa kazi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Heshima wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji (Mo Dewji) amemkaribisha Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ambapo amemuahidi kumpa ushirikiano mkubwa.

Baada ya kuitembelea kambi mjini Dubai, Mo Dewji amemuahidi Kocha Robertinho kuwa katika dirisha la usajili atamuongezea wachezaji wengine wazuri ili aweze kutimiza malengo yake na klabu.

“Binafsi nakukaribisha sana Simba, tunaamini uzoefu wako na dhamira yako kwa timu, sisi tutakupa ushirikiano mkubwa na tutakuongezea wachezaji wapya katika dirisha hili la usajili ili uifanye kazi yako kwa usahihi,”amesema Mo Dewji.

Katika mazungumzo yake na benchi la ufundi, Mo Dewji amempongeza na kumshkuru Kocha Juma Mgunda kwa kukubali kuichukua timu katika nyakati ngumu na ameweza kuifanya kuwa imara zaidi.

Katika hatua nyingine, Mo Dewji amewashukuru wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wanaomaliza muda wao na amewatakia heri wanachama kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Januari 29, mwaka huu.

“Ninamshukuru Afisa Mtendaj Mkuu wetu, Barbara Gonzalez kwa kazi nzuri aliyoifanya ninaaamini ataendelea kuwa Simba na sisi tutaendelea kumpa ushirikiano,”amesema Mo Dewji.

Wakati huo huo, Mo Dewji amewataka wachezaji kutosikiliza maneno ya watu kuhusu yeye, kwani bado yupo sana na anawapenda na anaipenda Simba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news