Simba SC yajivunia kambi ya siku nane Dubai

NA DIRAMAKINI

MENEJA Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kambi ya siku ya nane waliyofanya mjini Dubai ilikuwa na mafanikio kwa kuwa Kocha Mkuu Roberto Oliviera (Robertinho) alipata muda wa kukaa pamoja na wachezaji.
Ahmed amesema baada ya Robertinho kukaa na wachezaji amewasoma tabia zao za ndani na nje ya uwanja, hivyo itakuwa faida kwake kuwaongoza katika mechi za mashindano.

Kuhusu mechi mbili za kirafiki walizocheza Ahmed amesema zilikuwa kipimo kizuri kwao si tu kwa michuano ya ndani bali hadi Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itaendelea mwezi ujao.
“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumerejea salama jijini Dar es Salaam na tutashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mbeya City kwenye Ligi Kuu ya NBC.
“Kambi yetu ilikuwa ya mafanikio mjini Dubai Kocha Robertinho amepata nafasi ya kukaa na wachezaji pia tumepata mechi nzuri za kirafiki ambazo zimetuonyesha mahali kikosi chetu kilipo kuelekea michuano iliyo mbele yetu,” amesema Ahmed.

Post a Comment

0 Comments