Haya hapa majina 1,738 ya Watanzania walioitwa kwenye usaili wa nafasi za ajira kupitia Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji na Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar

NA GODFREY NNKO

IDARA ya Uhamiaji imewatangazia vijana mbalimbali kama walivyoorodheshwa hapa chini waliotuma maombi ya nafasi za ajira kupitia Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, kufika kwenye usaili utakaofanyika katika Ukumbi wa Café Theatre 1 & 2 Ndaki (Faculty) ya Biashara na Uchumi Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) siku ya Jumamosi tarehe 28 Januari, 2023 saa 1:00 kamili asubuhi.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 18, 2023 na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dkt. Anna Makakala ambapo amefafanua kuwa,kwa wale waliotuma maombi kupitia Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar,wanatakiwa kufika katika ukumbi wa Dkt.Ali Mohamed Shein uliopo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja siku ya Jumamosi tarehe 28 Januari, 2023 saa 1:00 asubuhi.

"Waombaji wote wanatakiwa kufika na Vyeti halisi vya Kuzaliwa, Cheti cha Kidato cha Nne, Cheti cha Kidato cha Sita, Cheti cha Shahada, Cheti cha kuhitimu Mafunzo ya Awali ya Kijeshi kutoka JKT/JKU, Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA),kalamu ya wino ya buluu, vyeti vingine vya Kuhitimu Mafunzo katika fani mbalimbali ngazi ya Astashada na Stashahada,"amefafanua Dkt.Makakala.

Aidha, ameendelea kufafanua kuwa, kwa waombaji ambao muundo wa fani zao unatakiwa kusajiliwa na Bodi za Taaluma, wanatakiwa kufika na Vyeti halisi vya Usajili pamoja na leseni za kufanyia kazi kwa fani husika.

"Mara baada ya usaili wa awali kumalizika,Waombaji wa fani za Udereva, Ufundi wa Magari na TEHAMA wataendelea na Usaili kwa Vitendo siku inayofuata ya tarehe 29 Januari, 2023. Aidha, wasailiwa wote wanatakiwa kujigharamia chakula, usafiri na malazi wakati wote wa zoezi la usaili,"amefafanua.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wote wanapaswa kuvaa mavazi rasmi na nadhifu yenye heshima wanapokwenda kwenye usaili.

"Atayevaa nguo za kubana au fupi, jeans, t-shirt, kaptula na tracksuit hataruhusiwa kuingia kwenye usaili.Mwombaji yeyote atakayebainika kuwasilisha nyaraka za kughushi atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani,"amefafanua kupitia taarifa hiyo.

WANAOITWA KWENYE USAILI KUPITIA OFISI YA KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI MAKAO MAKUU DODOMA, WATAKAOFANYA USAILI KATIKA UKUMBI WA CAFÉ THEATRE 1 & 2, CHUO KIKUU CHA DODOMA;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news