Simba SC yampa kandarasi Kocha Msaidizi kutoka Tunisia

NA DIRAMAKINI

UONGOZI wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam umefikia makubaliano ya kumwajiri, Ouanane Sellami (42), raia wa Tunisia kuwa kocha msaidizi kwa mkataba wa miaka miwili.

Sellami ni mapendekezo ya Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ambapo ataungana na Juma Mgunda kuongoza benchi la ufundi.

Sellami ana Shahada ya Uzamili ya Elimu ya Viungo ya Michezo kutoka Taasisi ya Superieur Education Sportive Sfax ya nchini Tunisia.

Aidha, Sellami ni kocha mwenye uzoefu na ana Leseni B kutoka Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) na kabla ya kujiunga na Simba SC alikuwa akiifundisha Timu ya Almadina ya Libya kwa mwaka 2022 na mwaka mmoja nyuma alikuwa akiinoa Gabesien inayoshiriki Ligi Daraja la pili Tunisia.

Ujio wa Sellami katika kikosi hicho unaelezwa ni kuliongezea nguvu benchi la ufundi kwa ajili ya michuano ya ndani pamoja na Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news