Chama awashukuru waliomuwezesha kupata tuzo

NA DIRAMAKINI

KIUNGO mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama amewashukuru wote waliomuwezesha kupata tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Desemba (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Chama ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya pili msimu huu baada ya kuwashinda nahodha John Bocco na Shomari Kapombe ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

“Kwanza namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufika hapa, naishukuru familia yangu kwa kunitia moyo, nawashukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano walionipa uwanjani na mashabiki walionipigia kura.

“Tuzo hii inaongeza hamasa kwa wachezaji ya kuipambania timu, kila mmoja anafanya jitihada za kuipata na hilo ni jambo zuri kwa timu,”amesema Chama.

"Ni mara ya pili msimu huu kuchukua tuzo hii, lengo langu ni kuchukua tena na tena kwa kuwa mpira ndio kazi yangu na nipo hapa kuisaidia Simba,”amesema.

Chama amekabidhiwa tuzo na pesa taslimu shilingi milioni 2,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

Katika mwezi Desemba, Chama alicheza dakika 540 akifunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa mengine saba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news