Songwe wajiandaa kimkakati kupaisha Sekta ya Utalii

NA DIRAMAKINI

MKOA wa Songwe upo katika mikakati thabiti ya kuhakikisha inavumbua vivutio mbalimbali vya kitalii ambavyo itaviendeleza kwa ustawi bora wa sekta hiyo ngazi ya mkoa na Kitaifa.

Hayo yamesemwa leo Januari 4, 2023 na mkuu wa mkoa huo, Mheshimiwa Waziri Kindamba baada ya kufanya ziara katika baadhi ya vivutio vya kitalii vilivyopo mkoani humo.

"Tunaibua vivutio vya kiutalii na kujua tulipotoka tujue tunapotoka kwenda, tumekuja huku kujifunza na kuviibua.Tunataka kujenga uchumi kupitia sekta ya utalii," RC Kindamba amesema.

RC Kindamba katika ziara hiyo ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa, Happiness Seneda,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi, Mheshimiwa George Musyani, viongozi wa dini na wengineo.

Kiongozi huyo na ujumbe wake wametembelea michoro na unyayo wa kale Nkangamo wilayani Momba, majimoto Kata ya Nanyala na kimondo cha Ndolezi Kata ya Mlangali vyote vilivyopo Wilaya ya Mbozi.

Wakati huo huo, Mkuu huyo wa mkoa ametaja mambo ambayo yataweza kusaidia mkoa huo kufungua uchumi kupitia utalii kuwa ni pamoja na kuboresha moundombinu, kuweka mikakati ya uchumi na kuibua vivutio hivyo na kuvitangaza zaidi.

"Tumetembelea vivutio ili kuviibua na kuvitangaza ili Dunia na Tanzania wajue Songwe tuna aina gani ya vivutio. Japo kwa uchache watu wavione maana kwa ujio wao fursa za kiuchumi zitafunguka.Tumeona changamoto hasa barabara tutaongea na watu wa TARURA (Wakala wa Barabara Vijijini) ili tuweze kutengeneza moundombinu ikae vizuri,"ameeleza Mheshimiwa Kindamba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news