Tozo ya kitanda nyumba za wageni ipo kisheria-TRA

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Geita imewataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni kuzingatia malipo ya tozo ya kitanda kwani ipo kwa mjibu wa sheria.
Hayo yameelezwa Januari 11, 2023 na Ofisa Elimu ya Mlipa Kodi na Huduma kwa Mteja TRA Geita, Justine Katiti alipokuwa akizungumza na wamiliki wa nyumba za kulala wageni mjini Geita.

Amefafanua, tozo ya kitanda ni mojawapo ya vyanzo vya mapato ya kuendeleza utalii inayolipwa kutoka malipo ya mgeni kwa usiku mmoja au sehemu ya siku kwenye nyumba ya wageni iliyosajiliwa.

Amesema, wamiliki wa nyumba za kulala wageni hawapaswi kulalamika kwani inatozwa kwa mujibu wa kifungu cha 59 cha Sheria ya Utalii ya mwaka 2008, hivyo kila mhusika awajibike.

“Ni lazima muelewe, tozo hii inatozwa kwa asilimia moja tu ya bei ya chumba, na inatozwa kwa kuzingatia bei halisi na siyo bei pungufu ya makubaliano yeyote, baina ya mmiliki na mteja,”amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news