Rais Dkt.Samia aanza kutekeleza ahadi yake BBT, ni neema kwa kila Mtanzania

NA MWALIMU UDADIS

HAYAWI hayawi sasa yamekuwa, mpango wa kuwawezesha vijana kwa kuwapa ujuzi na mahitaji ya kuwawezesha kuanza shughuli za kilimo umeanza rasmi kwa wote wenye uhitaji wa kujiajiri kutuma maombi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa DktSamia Suluhu Hassan anauanza mwaka huu 2023 kwa kasi ya 5G.

Wakati suala la ajira likiwa changamoto katika nchi zote za Afrika, Rais Samia ameweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza kuja na mwarobaini wa suala la ajira kwa kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo. Mpaka sasa zimetengwa takribani hekari 162,492.
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi thabiti wa Rais Samia imejikita katika kuwawezesha wananchi zaidi.

Katika hatua ya kwanza mashamba yametengwa katika mikoa ifuatayo; Mbeya (Hekari 52,165), Dodoma (Hekari 20600), Kagera (Hekari 3227) na Kigoma (Hekari 86500). Mpango wa BBT ni endelevu na utafika kila kona.

Sanjari na uwezeshaji huu, serikali inaendelea kutoa pembejeo kwa wakulima wote, msamaha wa kodi kwa malighafi za kilimo, kuiwezesha Bodi ya Nafaka kwa fedha za kutosha, kutafuta masoko ya kimataifa, kuwawezesha Maafisa Ugani nchi nzima, kuboresha miundombinu ya usafirishaji wa mazao na kudhamini tafiti muhimu kwa sekta ya kilimo.

Tanzania ina ardhi nzuri inayofaa kwa kilimo takribani Hekta Milioni 13 na nusu, hivyo uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan utakuwa wa kihistoria na wenye kumgusa kila mtanzania moja kwa moja au vinginevyo, hususani vijana.

MUNGU MMBARIKI RAIS WETU, MUNGU IBARIKI TANZANIA YETU

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. Mama anaupiga saaana lakini tulioomba hatujui majina watatoa lini maana walitangaza kuwa mafunzo ni tar 15 feb hii imekaaje ?

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news