Uongozi wa NHC wapewa kongole, watakiwa kulipa kodi kwa wakati na kutunza majengo

NA GODFREY NNKO

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu ameendelea kupongezwa kwa namna ambavyo anashirikiana na watumishi wenzake ndani ya shirika hilo kufanya kazi kwa bidii, kubuni na kutekeleeza miradi yenye tija kubwa kwa shirika, jamii na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa Januari 27, 2023 na Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano KingJada Hotels & Apartments Ltd, Morocco Square jijini Dar es Salaam,Risasi Mwaulanga wakati uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na KingJada Hotels and Apartment Ltd wakisaini mkataba wa kihistoria kwa ajili ya upangishwaji na uwekezaji wa ubia kwa ajili ya huduma ya hoteli katika Mradi wa NHC Morocco Square jijini Dar es Salaam

"Siku hii ya leo ni siku ya kihistoria kuona fungamano la kiuchumi likifanyika katika ushuhuda ambao unahitaji matokeo chanya yenye faida ya kiuchumi na maendeleo yetu.

"Ili haya yote yaweze kufanyika nitakuwa mchoyo wa fadhila kama hatutaweza kumpongeza kiongozi mwenye fadhila na mchapakazi, Nehemiah Mchechu,watumishi na menejimementi nzima ya NHC.

"Ninazungumza hivi kwa sababu taifa lolote duniani hutumia rasilimali watu na rasilimali maliasili ili kuleta maendeleo ya maeneo yake na watu wake kwa uchumi ulio bora, sasa kwa kuwa na Nehemiah Mchechu ambaye ni mzalendo kwa maneno yake ametuhakikishia kwa vitendo vyake, kama unavyoona miradi mikubwa namna hii.

"Nani sio shuhuda hapa anavyoona nyumba salama Tanzania nzima zikikua kwa kasi, kwa makazi ya watu wa hali ya juu, hali ya kati na sisi watu wa Kimbangulile. Mimi ninakaa Kijichi Mbagala, kuna nyumba za NHC ni accommodation ambao zimetuwezesha na sisi kupata makazi bora kabisa, tunajivunia kwa jambo hilo wakazi wa Mbagala,"amefafanua Mwaulanga.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mkuu huyo amesema, KingJada Hotels wanayo imani kubwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

"Hivyo ni rai yetu kwetu wote wakiwemo wadau wote wa kibiashara kuhakikisha tunaofanya ubia wa biashara na shirika letu la NHC kuhakikisha tunafuata taratibu na sheria zilizowekwa kwa mujibu wa mikataba yetu.

"Sisi tunayo imani kwamba shirika litafika mbali kimalengo na kimkakati na pia na sisi wabia kufikia malengo ya kibiashara iwapo tunafuata kanuni na sheria zilizowekwa kwa mujibu wa mikataba yetu, lakini pia tuwe mabalozi na wenye mapenzi mema na shirika hili kwa kulipa kodi kwa wakati na sisi pia kutunza majengo haya ya kibishara na makazi tuishi kwa vission na mission ya NHC,"amesisitiza Mkurugenzi Mkuu huyo wa Mawasiliano KingJada Hotels.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news