Uzeni nyama ambazo zimegongwa mihuri toka mamlaka husika-Polisi

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi nchini kupitia Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo limewataka wafanyabiashara wa kuuza nyama kuhakikisha wanauza nyama ambazo zimegongwa mihuri toka mamlaka zinazohusika.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua leo Januari 18,2023 wakati alipotembelea mabucha ya kuuza nyama katika Soko Kuu la Arusha.

ACP Pasua amewataka wauza nyama wote kuhakikisha wanafuata kanuni na taratibu zinazowaongoza sambamba na kuuza nyama ambazo zinatoka katika machinjio ya Serikali ambapo mifugo inapimwa kabla ya kuchinjwa.

Naye Mkuu wa soko hilo, Datus Renatus mbali na kupongeza Jeshi la Polisi amesema, wamejifunza mambo mengi kupitia maelekezo mbalimbali ambayo wameyapata kutoka Polisi ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara wa nyama kuhakikisha wanafuata kanuni na taratibu za biashara zao.

Mwenyekiti wa Mabucha Soko kuu la Arusha, Ezekiel Michael amesema wamepokea changamoto ambazo wameambiwa na kuhaidi kuzifanyia kazi lakini pia akawataka wafanyabiasha wa nyama kucha tabia ya kununua mifugo ya wizi badala yake wanunue ile ambayo imefuafa taratibu.

Naye Laban Kivuyo ambaye ni muuza nyama katika soko hilo ameliomba Jeshi la Polisi kuendelea kuwa karibu nao kwani kupitia ukaribu huo taarifa nyingi za kihalifu zitaripotiwa.

Pia amewataka wafanyabiashara wanaopokea mali za wizi hasa mifugo kuacha tabia hiyo kwani Serikali ipo makini badala yake wafanye kazi zinazotambulika kisheria zitakazowaingizia kipato halali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news