Waziri Dkt.Tax:Nimejionea, kazi bado ni kubwa inabidi muongeze bidii zaidi

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt.Stergomena Tax (Mb), ametembelea na kujionea namna ujenzi wa jengo la wizara katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma unavyoendelea.
Katika ziara hiyo ya ukaguzi, Mhe.Dkt.Tax amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa jengo hilo kuongeza kasi ili ujenzi ukamilike kwa wakati.

“Nimetembelea hapa, nimejionea kazi ilipofika, kazi bado ni kubwa inabidi muongeze bidii zaidi ili Mungu akijaalia mwezi Oktoba mwaka huu badala ya Desemba ujenzi uwe umekamilika na tuone tunajipanga namna gani,”amesema Dkt.Tax.
Mhe. Dkt.Tax kwa pamoja na Mhe.Balozi Mbarouk wakiingia kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Amesema, wizara ina uhitaji mkubwa wa jengo hilo kwa kuwa watumishi wametawanyika katika maeneo matatu tofauti na inakuwa ngumu kukutana kwa haraka pale inapobidi.
Amesema kukamilika kwa jengo Hilo kutatoa ahueni kwa watumishi wa wizara na kuwawezesha kuwa sehemu moja na hivyo kurahisisha utendaji kazi wa Wizara.

Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Dkt. Tax aliambatana na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine na watendaji wengine wa Wizara.
Mkandarasi wa Jengo la Wizara akifafanua jambo kwa Mhe. Dkt.Tax kuhusu hatua mbalimbali za ujenzi wa jengo hilo kwa kuonesha picha.

Ujenzi wa jengo la Wizara ulianza mwezi Januari 2022 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2023. Ujenzi huo utagharimu kiasi cha Shilingi bilioni 22.9 ambazo zimetolewa na Serikali ili kuziwezesha Wizara na Taasisi za Serikali kuwa na majengo ya kudumu katika mji wa Serikali.
Ujenzi huo unafanywa na umoja wa makampuni ya Sole Works na mshauri elekezi ambaye ni Chuo Kikuu cha Ardhi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news