Waziri Mchengerwa atengeua teuzi tatu, amteua Addo November kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amemteua Addo November kutoka kwenye tasnia ya muziki nchini kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa nchini kwa lengo la kuimarisha utendaji na ufanisi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 26, 2023 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, John Mapepele imefafanua kuwa, Mheshimiwa Mchengerwa amefanya uteuzi huo kwa mamlaka aliyonayo.

Ni kwa mujibu wa Ibara ya 3 Kifungu cha 3.1 cha Katiba ya mfuko huo, ambapo uteuzi huo unaanza leo na utadumu kwa miaka mitatu.

Aidha, Mheshimiwa Waziri Mchengerwa ametengua uteuzi wa wajumbe watatu wa mfuko huo baada ya kukosa sifa ya uwakilishi wa makundi mahsusi ya kisekta waliyoyawakilisha wakati wa uteuzi wao kwa maslahi mapana ya Taifa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wajumbe hao ni Bi.Frida James Kombe, Bw. Godfrey Baltazar na Bw. Salum Mbaruku Twiza.

Post a Comment

0 Comments