Yanga SC yaimarisha safu ya ukabaji

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imeimarisha safu yake ya ukabaji baada ya kuingia kandarasi ya miaka miwili na kiungo wa zamani wa Azam FC,Mudathir Yahaya.
Yahaya ambaye anatajwa kuwa ni chaguo la Kocha Mkuu wa Yanga SC,Prof.Nasreddine Nabi anaungana na viungo wewngine wakabaji akiwemo Gael Bigirimana Zawadi Mauya, Khalid Aucho na kiraka Yannick Bangala.

Pengine huu unaweza kuwa, usajili bora zaidi kupitia dirisha dogo ambao Yanga SC wamefanya mwanzoni kabisa mwa mwaka mpya.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ndiyo wanaoongoza msimamo wa ligi hiyo kwa alama 50 za michezo 19.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news