Hii hapa orodha ya majina 812 ya vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya kilimo kupitia Programu ya BBT-YIA Februari, 2023

NA DIRAMAKINI

SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo inatekeleza Programu ya Kuwezesha Ushiriki wa Vijana katika Kilimo Biashara (Building a Better Tomorrow Youth Initiative for Agribusiness (BBT-YIA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Januari 10, 2023 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ilifafanua kuwa, programu hii inatarajiwa kuongeza ajira kwa vijana kufikia milioni tatu (3) na kuongeza ukuaji wa sekta ya kilimo hadi kufikia asilimia10 ifikapo mwaka 2030 (Ajenda 10/30).

Aidha, kupitia BBT, Wizara inaratibu uanzishwaji wa mashamba makubwa ya pamoja (Block Farms) kwa ajili ya vijana.

Mradi huu utatekelezwa nchi nzima na vijana wote wenye sifa watapata fursa ya kufanya kilimo biashara katika mnyororo wa thamani.

Kwakuanzia, Wizara imetambua mashamba yenye jumla ya ekari 162,492 katika Wilaya ya Chunya (Mbeya); Bahi na Chamwino (Dodoma); na Misenyi na Karagwe (Kagera); na Uvinza na Kasulu (Kigoma).

Hivyo, wizara ilitangaza fursa za mafunzo ya kilimo biashara kwa awamu ya kwanza kwa vijana katika Kituo cha Mafunzo ya Kilimo Bihawana mkoani Dodoma.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza hivi karibuni ambapo vijana watapatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu. Baada ya mafunzo hayo, wahitimu watakabidhiwa mashamba kwa ajili ya kilimo kwa taratibu na masharti yatakayoainishwa.

Majina hapa chini ni sehemu ya maombi ambayo yalitumwa kupitia kiunganishi cha bbt.kilimo.go.tz kuanzia Januari 10, 2023. Na mwisho wa kutuma maombi ulikuwa ni Januari 30, 2023.

Sifa za vijana waliotakiwa kuomba ni pamoja na:-
i. Awe Mtanzania;
ii. Awe na umri kati ya miaka 18 - 40;
iii. Awe anapenda kufanya kilimo biashara; na
iv. Awe anashiriki kwenye shughuli za kilimo.

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA KILIMO KUPITIA PROGRAMU YA BBT-YIA FEBRUARI, 2023;














Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. NashaUli wapate elimu hiyo Kisha waludi mkufanyia kazi nawape fursa wengine kujifunza hii ingepanua wigo kwenye kilimo

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news