IRUWASA yavuka lengo Sera ya Maji, ilani ya chama tawala

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA) imevuka lengo la sera ya maji na ilani ya chama tawala ya kutoa huduma ya usambazaji maji kwa mji wa Iringa na maeneo ya pembezoni inayowafikia wakazi mkoani humo kwa asilimia 97.

Mkurugenzi Mtendaji wa IRUWASA,Mhandisi David Pallangyo ameyabainisha hayo leo wakati akielezea mafanikio ya mamlaka hiyo mbele ya waandishi wa habari jiijini Dodoma.

Amesema, IRUWASA imefanikiwa kuhakikisha huduma ya maji Mjini Iringa na maeneo ya pembezoni inapatikana kwa wastani wa saa 23 kwa siku na imefanikiwa kuongeza ukusanyaji maduhuli kwa huduma zilizotolewa kutoka wastani wa shilingi milioni 770 mwaka 2020 kwa mwezi hadi shilingi milioni 860 kwa mwaka 2023.

Mhandisi Pallangyo amesema, hali hii inaiwezesha IRUWASA kuweza kugharamia kwa kiasi kikubwa uendeshaji wa taasisi tumefanikiwa kupunguza kiasi cha maji yasiyolipiwa (NRW) kwa upande wa Iringa Mjini kutoka wastani wa 24.6 (2020) hadi wastani wa 22.52% (mwezi Desemba, 2022).

Pia idadi ya wateja au maunganisho ya majisafi imeongezeka kutoka 28,133 (2020) hadi 40,549 (Desemba, 2022).

Amesema, IRUWASA imefanikiwa katika eneo la TEHAMA kwa kufunga mita za malipo kabla kwa wateja 6,752 na kuwa mamlaka inayoongoza nchini kwa kufunga mita nyingi za maji za malipo kabla.

Mhandisi hiyo amesema, mamlaka imendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji kwenye Miji ya Ilula na Kilolo pamoja utekelezaji wa mradi wa Isimani-Kilolo ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2023.

Amesema, pamoja na mafanikio hayo IRUWASA inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji, shughuli za kibinadamu zinazofanyika katika vyanzo vya maji kama vile kilimo, ufyatuaji wa matofali.

Nyingine ni mifugo, ukataji miti, uchimbaji wa mchanga au mawe vimekuwa changamoto kubwa kwani vimekuwa vikipelekea kupungua kwa kina cha mto Ruaha mdogo hasa wakati wa kipindi cha kiangazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news