Mchungaji Victoria:Dkt.Nabiijoshua Aram Mwantyala ni Rais mnyenyekevu, mzuri mwenye hekima

NA DIRAMAKINI

MCHUNGAJI Victoria Joseph kutoka Chuo cha Biblia cha Life Centre International,na Mweka Hazina wa Umoja wa Mitume na Manabii Tanzania (UMMT) Mkoa wa Kilimanjaro amesema kuwa, ataendelea kusimama imara na uongozi wa umoja huo chini ya Rais Dkt.Nabiijoshua Aram Mwantyala.

Dhamira ya umoja huo ambao unalenga kuwaleta pamoja mitume na manabii kwa ajili ya kueneza habari njema ya neno la Mungu nchini, kuombea, kuwezeshana, kuwezesha wenye mahitaji mbalimbali pia umekusudia kushirikiana na Serikali kuhakikisha wanatekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Hivi karibuni,Dkt.Nabiijoshua Aram Mwantyala ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania alitwaa asilimia 80 ya kura katika uchaguzi wa nafasi ya urais katika Umoja wa Manabii na Mitume nchini Tanzania (Unity of Apostles and Prophets Tanzania).

Ushindi huo ulitokana na kura 179 alizopata huku akiwaacha mbali washindani wake akiwemo Mchungaji Ceasar Masisi aliyepata kura 42 na Mtume Joackim Kimanza aliyepata kura nne kupitia uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Anatoglo uliopo Ilala, Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, Askofu Profesa Rejoice Ndalima alimtangaza rasmi Dkt.Nabiijoshua Aram Mwantyala kuwa Rais wa Umoja wa Mitume na Manabii nchini Tanzania.

Aidha, mitume na manabii mbalimbali nchini walionesha imani kubwa juu ya Dkt.Nabiijoshua huku wakimpongeza na kuahidi kumpa ushirikiano mkubwa aweze kutekeleza jukumu lake la kuwaunganisha viongozi hao wa kiroho ili waweze kulihubiri neno la Mungu kwa ufanisi nchini

"Ninaamini katika umoja, ninaamini kwa sababu Yesu alisema kwamba, tuwe na umoja kwa sababu hiyo ninasimama pamoja na Umoja wa Mitume na Manabii Tanzania chini ya Rais wetu, Rais mnyenyekevu, Rais mzuri mwenye hekima Joshua Aram Mwantyala.

"Ni Nabii wa Mungu wa hapa Tanzania, ninasimama na wewe Baba na pamoja na uongozi wote na jopo lote Tanzania, Mungu awabariki sana,"amefafanua Mchungaji Victoria Joseph.

Umoja wa Mitume na Manabii Tanzania (UMMT) unaongozwa na Rais Dkt.Nabiijoshua Aram Mwantyala ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania yenye makao yake makuu mjini Morogoro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news