Mkatekeleze kikamilifu majukumu yenu mikoani-Waziri Kairuki

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki leo Februari 28, 2023 Mtumba jijini Dodoma amekutana na kuzungumza na wakuu wa mikoa wapya na kuwakabidhi vitendea kazi.
Wakuu wa mikoa hao ni Mhe. Dkt. Francis K. Michael ambaye ni Mkuu wa Mkoa Songwe na Mhe. Christina S. Mndeme Mkuu wa Mkoa Shinyanga.

Waziri Kairuki amewata wakuu waikoa hao kutekeleza kikamilifu majukumu yao ili kutimiza azma ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaamini ili kumwakilisha katika mikoa hiyo.
Aidha, Waziri Kairuki amewataka wakuu wa mikoa kushirikiana na watendaji wote katika maeneo yao ili kuhakikisha kipaumbele cha Serikali kinachukua nafasi ya kwanza ili kuendana na utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Pia amewataka kujikita kutatua kero za wananchi katika maeneo yapo mara zinapojitokeza au kuwasilisha kwenye mamlaka husika ili ziweke kutafutiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news