MKUTANO WA KAWAIDA WA 43 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC KUFANYIKA BURUNDI

NA MWANDISHI WETU 

MKUTANO wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unatarajiwa kufanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 23 Februari 2023.
Mwenyekiti wa Mkutano wa majadiliano kwa ngazi ya wataalam kutoka Burundi (kushoto) akiongoza kikao hicho kilichofanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 19 Februari 2023 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Masahriki unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 Februari 2023. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango na Utawala, Mhandisi Steven Mlote.
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa majadiliano kwa ngazi ya wataalam uliofanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 19 Februari 2023 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Masahriki unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 Februari 2023. Mkutano kwa ngazi ya wataalam unafanyika kuanzia tarehe 19 hadi 20 Februari 2023 na utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu tarehe 21 na 22 Februari 2023. Kulia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Haji Janabi.
Mkutano huo ambao umeanza kwa Ngazi ya Wataalam tarehe19 hadi 20 Februari 2023 utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 21 na 22 Februari 2023 na kuhitimishwa na Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 23 Februari 2023.
Ujumbe wa Burundi ukishiriki Mkutano wa Ngazi ya Wataalam unaofanyika jijjini Bujumbura, Burundi kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa EAC. Burundi ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kiongozi wa Ujumbe wa Rwanda akishiriki Mkutano wa Wataalam.
Ujumbe wa Uganda ukishiriki Mkutano huo

Mkutano wa Wataalam utapitia na kujadili agenda mbalimbali muhimu kuhusu masuala ya mtangamano wa Jumuiya hiyo ambazo baadaye zitawasilishwa kwenye Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 21 na 22 Februari 2023 kwa majadiliano na hatimaye agenda hizo zitawasilishwa kwenye Mkutano ngazi ya Mawaziri unaotarajiwa kufanyika jijini hapa tarehe 23 Februari 2023.

Miongoni mwa agenda hizo ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa kwenye vikao vilivyopita katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara na forodha, miundombinu, ulinzi na usalama, sheria, utalii, ajira na utawala na fedha; Kupokea taarifa ya mwaka ya Ukaguzi wa Hesabu za Jumuiya kwa mwaka wa fedha ulioishia mwezi Juni 2022; Taarifa ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya; Taarifa kuhusu Taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kupitia na kupitisha ratiba ya shughuli za Jumuiya kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2023.
Ujumbe wa Kenya nao ukiwa katika Mkutano.
Kiongozi wa Ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nae akishiriki mkutano wa wataalam.
Wajumbe kutoka Taasisi za Jumuiya ya Afrika wakishiriki mkutano wamaandalizi ya mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa EAC.
Wajumbe kutoka Sekreatarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakishiriki Mkutano wa Wataalam jijini Bujumbura.
Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Sera, Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi Agnes Meena akishiriki Mkutano wa Wataalam.
Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Bernard Haule akishiriki mkutano wa wataalam.
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakishiriki Mkutano wa Wataalam.
Sehemu ya Wajumbe wa Sekretarieti ya EAC wakifuatilia mkutano.
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe kutoka Tanzania katika mkutano.
Mkutano ukiendelea.

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Ngazi ya Wataalam unaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi. Ujumbe huo pia unajumuisha Wajumbe kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Katiba na Sheria.

Kadhalika Mkutano huo umehudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi zote wanachama ambazo ni Burundi ambaye ni mwenyeji wa mkutano, Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini ambao wameshiriki kwa njia ya mtandao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news