Viingilio kati ya Simba SC, Azam FC vyatajwa

NA DIRAMAKINI

BAADA ya mazoezi ya jana kikosi cha Simba SC kimeingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya Azam FC utakaopigwa kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo, wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna yoyote ambaye amepata maumivu yatakayomfanya kukosa mchezo wa kesho.

Aidha, baada ya mchezo wa juzi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca, jana Simba walianza maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam moja kwa moja na lengo ni kuhakikisha wanashinda.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viingilio vya mchezo ni mzungo shilingi 5000, VIP B na C na shilingi 10,000 huku VIP A ikiwa ni shilingi 15,000.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news