Ombeni (Ben) Pallangyo anavyotumia Ombeni African Safaris kuiheshimisha Sekta ya Utalii nchini

NA DIRAMAKINI

UKIFANIKIWA kumuuliza mtu yeyote ambaye amewahi kufanya utalii kutoka ndani na nje ya Tanzania, atakuambia kuwa, Tanzania katika eneo kubwa imekirimiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ambavyo vina upekee wa aina yake hapa Duniani.

Miongoni mwa vivutio hivyo ni Mlima Kilimanjaro, huu ni mlima mrefu zaidi barani Afrika. Tanzania ni inajumuisha watu zaidi ya milioni 60 wenye ukarimu, upendo na mshiakamano kwa kila mgeni.

Vile vile ina makabila 120 na zaidi ya lugha 126 tofauti. Kwa ujumla,mandhari ya kipekee ya Tanzania yanatoa taswira njema na mvuto wa aina yake katika Sekta ya Utalii barani Afrika.

Ili kuweza kuifahamu Tanzania na vivuto vyake, kuna wazawa ambao kwa kipekee wamejipa muda wa kujifunza na kuifahamu kwa kina nchi hii hususani upande wa vivutio vya utalii.
Miongoni mwao ni Ombeni (Ben) Pallangyo, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Ombeni African Safaris na Mwanzilishi na Mwenyekiti wa The Ombeni Foundation, mzaliwa wa Arusha ambaye anaufahamu vema uzuri wa Tanzania kupitia vivutio vya utalii.

Ombeni Pallangyo pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Banana House Garden Grill Arusha,Tandoori House Kitchen Arusha na The Bougainvillea Iliboru Kisiwani jijini Arusha.

Ben ametumia miaka mingi kufanya kazi katika sekta ya utalii na amesaidia kuchagiza jinsi inavyoonekana leo nchini Tanzania.

Akifanya kazi yake kupitia kampuni kuu za watalii katika Afrika Mashariki, yeye ni mtu anayeongozwa na kanuni zenye kuleta tija na matokeo chanya akizingatia utaalam na misingi ya kitaaluma.

Sifa hizi zimemsukuma mbele ya tasnia yake, pamoja na uzoefu wake katika utalii, wanyamapori, usimamizi wa hoteli na sanaa ya upishi. Kumwezesha kuwa mmoja wa waendeshaji watalii bora Afrika Mashariki.

"Tunaendelea kuongoza safari bora na za kukumbukwa nchini Tanzania na kwingineko," anasema, "tukifanya kazi na watu mbalimbali kutoka kwa wanandoa hadi makundi makubwa ya familia, maafisa wa serikali, watendaji wakuu wa makampuni na watafuta matukio."

Siri

Ben anajua thamani ya kuwashirikisha watalii katika vivutio ambavyo vitaweka historia ya kudumu katika maisha yao yote. Ndiyo maana, wageni na watalii wengi wa ndani na nje huwa wanapenda kufanya chaguo la kwanza kupitia huduma za Ombeni African Safaris.

"Ombeni African Safaris imeshinda tuzo kwa sababu nyingi, kwa sababu tunachukua watu nje kuibua vivutio visivyofahamika na vyenye upekee wa aina yake Afrika," Ben anasema, "Kama kampuni iliyozaliwa Afrika inayofanya kazi na timu bobezi ya wataalamu wa Afrika, tunaelewa ardhi hii kikamilifu na tunaweza kutoa huduma bora kwa wateja wetu."

Na ni mchanganyiko wa uzoefu huu na ubunifu ambao umewaweka mbele ya washindani wao. Kwani, Ben ameunda vifurushi vinavyohusisha fursa nyingi za kuketi na kuthamini thamani ya maoni na hadhi ya ardhi hii nzuri.
"Fikiria unaamka karibu kabisa na Mlima Kilimanjaro huku jua likitanda juu ya vilele vyake," Ben anaeleza, "Kisha kabla ya kitu chochote kile, siku huanza na harufu ya kahawa ya Robusta na Arabica kutoka kwenye mashamba ya familia ya Ombeni.

Ombeni African Safaris pia huwa inaratibu ziara nyingi katika vivutio vya kitalii na maeneo mbalimbali yenye mvuto wa aina yake nchini.

Ziara hizo za kipekee huwa zinaandaliwa ili kuruhusu wageni kuchagua mtindo wao wenyewe wa kutalii Tanzania na Afrika kwa ujumla. Huku suala la usalama, ukarimu na upendo ukiwa ndiyo msingi wa mambo yote.

Pia huwa na utaratibu muhimu wa kuwapa wageni wote ratiba ya shughuli za siku inayofuata yakiwemo mambo muhimu ya msingi katika maeneo waliyofikia.

Wasafiri

Jambo moja ambalo unaweza kuhakikishiwa na Ombeni African Safaris, ni kuwa na timu yenye morali na bidii katika huduma za utalii ambazo zitakuwezesha kupata safari binafsi au makundi.

"Tunawahimiza wageni wetu kufurahia vivutio vya utalii Tanzania na Afrika kwa njia ya Ombeni African Safaris," Ben anasema, na kuongeza, "Na kama hawataki kuitumia Ombeni African Safaris basi wako kwenye ziara isiyo sahihi. Wakati safari inapoanza tunageuza ndoto za safari kuwa ukweli na kutengeneza kumbukumbu za dhahabu kwa wageni wetu. Hili linahitaji ubunifu na uvumbuzi.”

Ben anaendelea kueleza kuwa, kutegemea timu yake kikamilifu ni sehemu ya mafanikio ya biashara. Kwa kuruhusu wafanyakazi wake kuwa na uhuru wa kubinafsisha ratiba yoyote ili ilingane kikamilifu na mteja ni muhimu ili kuwasaidia kujifunza kikamilifu katika utamaduni wa Kiafrika kwa njia ambayo ni ya kipekee kwa kila mmoja wao.

"Nani anataka kwenda safari ya kawaida? Bila shaka hayupo, ndiyo maana wengi wanajivunia Ombeni African Safaris, wabobezi katika mambo ya utalii ambao wanaifanya safari yako kuwa zaidi ya matarajio, bila shaka utafurahia na kujifunza zaidi."

Kwa kweli, kuna orodha ya mambo ambayo hufanya Ombeni African Safaris kuwa bora. Kwa mfano, wakati safari zinaweza kufanywa na vikundi vikubwa na vidogo, magari ya Land Cruisers hayajasongamana kamwe.

Ingawa kuna viti vya kutosha kwa watu wanane, huchukua watano tu kwa kila gari kuruhusu kila mtu kuwa na kiti chenye dirisha ili aweze kuona vivutio bora zaidi.

"Tunaamini kuwa watu wanataka kufurahia, kujifunza na kuviona vivuto vya utalii kwa ukaribu." Sehemu hii ya mwisho inavutia sana kwani kutokana na uzoefu wa timu bora barani Afrika na vile vile uhusiano wa kifamilia, kuna sehemu za bara ambazo ziko wazi kwao ambazo haziko wazi kwa kampuni zingine. Kuwapa wageni wao uzoefu wa kipekee wa safari.

Nyakati zisizosahaulika

“Fikiria ukungu wa asubuhi unaofunika Serengeti kama blanketi na jua likielea juu ya upeo wa macho huku utulivu wa amani ukikuzingira,” Ben anaeleza namna ambavyo safari za puto zilivyo na raha yake katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia huduma za Ombeni African Safaris.
Ben anaeleza kuwa,Kampuni ya Ombeni African Safaris imejizatiti kuwajibika katika usafiri huku ikiwekeza barani Afrika na kuliacha bara hilo mahali pazuri kwa vizazi vijavyo. Hii ni pamoja na kufanya kazi kwa mtindo endelevu, kufikiria kwa njia ya asili na kuendelea kuwa mfano katika sekta ya utalii ndani na nje ya Tanzania.

"Tunapaswa kufikiria na kuchukua hatua sasa ili kuhifadhi ulimwengu asilia tulionao kwa ajili ya vizazi vijavyo," anasema, "na tunaendelea kutafuta mawazo mapya kwa ajili ya Afrika ya Kijani."

Wakfu

Wakfu wa Ombeni (Ombeni Foundation) ni shirika lisilo la faida,linalojitolea kusaidia na kutoa mahitaji ya watu katika vijiji vya Meru na vingine nchini Tanzania.

Ben aliuanzisha wakfu huo ili kusaidia miradi mingi na kuhakikisha watu wanapata mahitaji ya kimsingi ya binadamu kama vile makazi, chakula, msaada wa matibabu na vifaa vya shule na michezo.

Sio mbali

Ben ambaye kwa sasa anaishi Madison, WI nchini Marekani, bado yuko karibu na asili yake ya kitamaduni na kifamilia katika nchi yake ya Tanzania.

Anaeleza kuwa, maisha yake yote na mafanikio yake yalichipuka kutokana na mizizi aliyoianzisha na analenga kurudisha tabasamu kijiji kilichomlea.

"Ninahisi kubarikiwa kila ninapowashirikisha fursa Watanzania wenzangu, nitaendelea kufanya hivyo mara zote nikiamini kuwa, asili yangu ni Mtanzania hivyo nitaendelea kufanya kazi kwa ustawi bora wa familia zetu huko nyumbani na Tanzania kwa ujumla." Unaweza kujifunza zaidi hapa katika tovuti ya Ombeni African Safaris;www.ombeniafricansafaris.com

Kwa Rais

Wakati huo huo, Ombeni Pallangyo amewataka Watanzania kuendelea kuthamini, kuheshimu na kuunga mkono kitendo cha kizalendo kilichofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimwa Dkt.Samia Suluhu Hassan cha kuandaa filamu maalumu ya Tanzania Royal Tour kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania Kimataifa.

Lengo likiwa ni kuwezesha Taifa kupata watalii wengi wa kigeni ambao watatoa mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi na kufungua fursa za ajira.

Filamu hiyo ya dakika 56 inaonesha vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania Bara kama vile Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengenti,na Tanzania visiwani inaonesha hoteli za kitalii ikiwemo iliyopo ndani ya bahari huko Pemba.

Aidha, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ndiye kiongozi wa kutoa maelezo kuhusu vivutio hivyo kwa Peter Grenberg, ambaye ni mwanahabari nguli na mtozi wa filamu kutoka kituo cha televisheni cha CNBC nchini Marekani.

Ombeni amesema kuwa,kitendo cha Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuamua yeye mwenyewe kuandaa filamu hiyo kwa kupita katika hifadhi za Tanzania ni uzalendo wa kipekee aliouonesha kwa lengo la kuhakikisha Sekta ya Utalii nchini inaleta mapinduzi thabiti ya kiuchumi kwa Watanzania.

Amesema, kwa sasa kila mmoja anashuhudia matokeo ya kazi hiyo nzuri aliyoifanya yaliyoanza kupatikana.

Ameongeza kuwa, ziara ya Rais Samia katika mataifa mbalimbali aliyofanya ikiwemo Marekani ambako pia Uzinduzi wa Filamu ya Tanzania Royal Tour ulifanyika umezidi kuleta tija na kila mmoja anashuhudia matokeo yake na mapokeo chanya ya filamu hiyo kimataifa, kitendo ambacho ni ujasiri na uthubutu mkubwa uliofanywa na Rais Samia kwa maslahi mapana ya nchi.

"Rais Samia ni hodari sana, nimpongeze kwa ujasiri wake mkubwa wa kupita mbugani akiandaa filamu hiyo, amefanya kazi ya mtu mwingine kwa upendo wake wa dhati.

"Wamepita Mawaziri wengi nyuma wa Utalii, lakini hawakufanikiwa kuleta mabadiliko kutokana na kutokuelewa, kuwajibika na ubishi. Jambo hili lingekuwa limefanyika huko nyuma, lakini ni uthubutu wa hali ya juu wa Rais Samia kuamua kufanya hivyo kwa manufaa ya nchi, lazima tumpongeze sana.

"Kitendo cha Mheshimiwa Rais kuacha ofisi na majukumu yake kufanya kazi ya mtu mwingine ili kuonesha mfano bora ni cha kupongezwa na kuungwa mkono. Lazima kuona utalii unakuwa endelevu na pia kuwa na watu ambao akili zao zimechambuka na pia wana connection na Sekta ya Utalii, lazima nguvu ipelekwe mataifa ya nje watu waliko na kuambatana na watu wanaojua tunakwenda wapi,"amesema Bw.Ombeni.

Amesisitiza kwamba ili kuzidi kufanikisha suala la kukuza utalii nchini, watu wanahitajika watakaozidi kujituma kwa moyo wa dhati wakitumia vyema maarifa yao, ubunifu, kujitambua, na ushupavu thabiti wa kutembea sambamba na Mheshimiwa Rais Samia katika kufanikisha kwa ufanisi ukuzaji wa utalii.

Ombeni ameziomba Balozi za Tanzania katika mataifa mbalimbali, zimsaidie Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka kipaumbele kuitangaza Tanzania na fursa zake katika kufanikisha kuifanya Sekta ya Utalii nchini izidi kuinufaisha Tanzania na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Wakati huo huo, Bw.Ombeni Pallangyo amewashauri baadhi ya watumishi wa umma ambao wana jukumu la kuunganisha na kuimarisha umoja miongoni mwa jamii kuendelea kuwajibika kwa uaminifu na uwazi ikiwemo kuacha kasumba ya kufanya kazi kwa mazoe na wakati mwingine kuyatazama maslahi yao.(thelostexecutive)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news