Prof.Muhongo:Dhamira ni kuhakikisha elimu inakuwa msingi mkuu Musoma Vijijini

NA FRESHA KINASA

KATIKA kuhakikisha kiwango cha ufaulu wa mitihani kwenye shule za sekondari za Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara unakuwa wa kuridhisha, Mbunge wa jimbo hilo, Prof. Sospeter Muhongo, aliitisha kikao kati yake na wakuu wa shule zote za sekondari 27 zilizopo jimboni humo.

Mbunge wa Musoma Vijijini, Mheshimiwa Prof.Sospeter Muhongo.

Kikao hicho kilifanyika Februari 3, 2023 katika Shule ya Sekondari Busambara katika Kijiji cha Kwikuba ambapo mahudhurio yalikuwa asilimia 92.6 kwa sekondari 25 kuhudhuria katika kikao hicho muhimu na sekondari mbili pekee hazikuhudhuria huku moja ikiwa ni ya binafsi.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini leo Februari 15, 2023 imeeleza kuwa, "sehemu ya kwanza tutaanza kwa kuonyesha ufaulu wa sekondari zetu kwa miaka mitatu mfululizo (2020-2022).

"Na sehemu ya pili ya taarifa itaeleza sababu za ufaulu wetu kutorodhisha, na mapendekezo ya uboreshaji wa mbinu za kujifunza na kufundisha yatatolewa,"imesema taarifa hiyo na kuonesha mtiririko wa ufaulu kwa miaka mitatu (2020-2022);
 
Form II (2020) 
 
Kata: Div I-III 10-41%, 
 
Binafsi 87%

Kata: Div IV-0 59-90%

Binafsi: 13%

Form IV (2020)


Kata: Div I-III 6-21%

Binafsi: 100%

Kata: Div IV-0 79-94%

Binafsi: 0%

Form II (2021)


Kata: Div I-III 7-40%

Binafsi: 66%

Kata: Div IV-0 60-93%

Binafsi: 34%

Form IV (2021)


Kata: Div I-III 5-29%

Binafsi: 83%

Kata: Div IV-0 71-95%

Binafsi: 17%

Form II (2022)


Kata: Div I-III 4-20%

Binafsi: 59%

Kata: Div IV-0 80-96%

Binafsi: 41%


Form IV (2022)


Kata: Div I-III 7-39%

Binafsi: 98%

Kata: Div IV-0 61-93%

Binafsi: 2%

Aidha, taarifa hiyo imebainisha kuwa, "Ufaulu wa shule zetu za Sekondari za Kata hauridhishi.Nini kifanyike kuboresha na kuongeza uelewa na ufaulu kwenye Sekondari zetu za Kata? Fuatilia sehemu ya pili ya taarifa ya mjadala huu."imeelezea taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news