Rais Dkt.Samia atoa pole ajali iliyoua watu 12 na kujeruhi 63 katika basi la Frester, atoa maagizo

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao katika ajali iliyoua watu 12 na kujeruhi huko Dodoma.
Ajali hiyo imetokea saa sita usiku wa kuamkia leo Februari 9, 2023 katika Kijiji cha Silwa Pandambili barabara kuu ya Dodoma - Morogoro huku chanzo cha ajali hiyo ikidaiwa ni dereva wa basi kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari.

"Nawapa pole wafiwa waliopoteza jamaa zao katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Silwa, Dodoma usiku wa kuamkia leo Februari 9, 2023 na kusababisha vifo vya watu 12. Mungu awarehemu Marehemu wote. Naviagiza vyombo vya dola kuongeza usimamizi wa sheria za usalama barabarani
Awali Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Remidius Mwema amesema majeruhi katika ajali hiyo wapo 63, wanaume 40 na wanawake 23.

Amesema, majeruhi 36 wapo katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo, majeruhi 27 walipelekwa katika kituo cha Afya cha Kibaigwa ambapo kati ya hao 16 walihamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu zaidi na wengine walipelekwa Dodoma kutokana na hali zao kuwa siyo nzuri.

Tazama orodha ya majina hapa chini majeruhi waliopo Morogoro;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news