Rais Ruto aahidi kuachilia fedha Serikali za kaunti

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Kenya,Mheshimiwa William Samoei arap Ruto amesema, Serikali imejitolea kutoa fedha kwa wakati kwa serikali za kaunti.
Picha na Ikulu.

Mheshimiwa Rais Ruto amesema, utekelezaji huo utasaidia kuharakisha ugatuzi na kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.

Rais amebainisha kuwa, vitengo vya utawala vilivyogatuliwa ndivyo kitovu cha maendeleo ya Kenya. Pia ameahidi kufanya kazi kwa karibu na kaunti na "kuongeza ushirikiano wetu", hasa katika kilimo, usalama, afya na makazi.
"Kuna mageuzi dhahiri ambayo yamekuja kupitia ugatuzi na kwa hivyo, lazima tuunge mkono kaunti," alisema Rais Ruto wakati akihutubia Mkutano wa Tisa wa Kitaifa na Uratibu wa Kaunti huko Naivasha, Kaunti ya Nakuru.

Naibu Rais Rigathi Gachagua, Mwenyekiti wa Baraza la Magavana Ann Waiguru, Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula, Spika wa Seneti Amason Kingi, Mwanasheria Mkuu Justin Muturi, Magavana, walikuwa ni miongoni mwa wageni wengine waliohudhuria.
Rais aliwataka viongozi hao kujitahidi kuimarisha maelewano kati yao, kuungana na kushirikiana mara kwa mara. Alieleza kuwa, utamaduni wa uadui, makabiliano na mashitaka ni wa kuvuruga na ubadhirifu hauna tija.

“Inachelewesha utekelezaji, inawanyima Wakenya haki yao ya kupata huduma, lazima tuwe na nia moja."
Bw. Gachagua alisema ni lengo la Serikali kuhakikisha ugatuzi unafaulu.Alibainisha kuwa, kupitia ushirikiano mzuri na wenye kujenga na Serikali ya Kitaifa, kaunti zina uwezo wa kuibadilisha Kenya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news