REA:Mheshimiwa Rais Dkt.Samia anataka miradi ikamilike kwa wakati

NA DIRAMAKINI

MKURUGENZI Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa maelekezo mahususi kwa walioshinda zabuni ya kusambaza umeme vijijini kuhakikisha wanafanya kazi zenye ubora kwa ufanisi, uaminifu na kufuata makubaliano yaliyofikiwa katika mikataba.

Mhandisi Saidy ameyasema hayo leo Februari 17, 2023 na UFM Radio ya jijini Dar es Salaam ambapo amebainisha kuwa,nishati hiyo itawafikia wananchi wengi nchini.

...Kauli ya Rais itasaidia sana, dhamira yake ilikuwa ni kutaka miradi ambayo inalenga kupeleka huduma kwa jamii isicheleweshwe kwa sababu ambazo si za msingi sana.

"Kama kuna haja ya kuchelewesha sababu inapokuwepo iwe ya kweli na ya uzito, hii ni miradi inakwenda kuinua maisha ya wananchi na Rais amesisitiza imalizike kwa haraka."

Mhandisi Saidy amesema, katika huo mradi ambao walisaini juzi ni nusu kwa nusu. "Tumesaini kandarasi saba, mikataba iko 14, lakini wakandarasi waliosaini wako saba, watano ni wakandarasi wa ndani na wa nje ni wawili tu, China Railway ya China na moja ya Tunisia ambayo bado inatoka Afrika vile vile."

"Wakandarasi watano ni Watanzania. Kila mkataba una muda wake wa kutekeleza, ule mradi wa kwenye vitongoji ni wa miezi 18, lakini mingine ni miezi 12, kwa sababu maeneo au wateja si wengi sana."

"Katika kutoa tenda zetu, tumetoa kwa kanda, yupo Mkandarasi ambaye yeye anashughulika na Dodoma, Singida na Morogoro kupeleka umeme kwenye vituo vya afya.

"Kuna wakandarasi wengi kwa wakati mmoja watakuwa saiti. Muhimu mwananchi yeyote anayeishi kijijini huyo tunamlenga, kilichofanyika ili Serikali iweze kwenda kwa awamu, mwanzo wakati REA inaanzishwa 2007 hata makao makuu ya wilaya yalikuwa hayana umeme, kwa hiyo makao makuu yote tulihakikisha yanapata umeme.

"Tukatoka hapo tukaingia vijijini na wakati tunatoka hapo bado miradi ya vitongoji inaendelea kama ambavyo awali nilisema,hii miradi ambayo nilisema hii miradi ambayo tunaita ni ya ujazilizi ule tuliosaini jana ni wa ujazilizi, ule ulikuwa wa fungu la pili B, kwa hiyo kuna miradi miwili ya ujazilizi imetangulia mbele ujenzi ya ujazilizi one na ujenzi ujalizi namba mbili fungu la pili 'A' kwa hiyo miradi ya vitongojini inaendelea.

"Kingine ambacho watu hawafahamu REA ni kifupi cha Rural Energy Agency, Wakala wa Nishati Vijijini hata suala la aina yenyewe ya nishati sisi hatuishii kwenye umeme, tunao wajibu kwenye nishati nyingine ndio maana kipindi cha miezi mitatu tulikwenda Azam Tv kueleza mpango wa wakala kuanza kusaidia upatikanaji wa nishati bora ya kupikia maeneo ya vijijini,"amefafanua.

Februari 14, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati akishuhudia utiaji saini mikataba ya kuimarisha gridi ya taifa na kusambaza umeme vijijini alisema, miradi hiyo yenye thamani ya shilingi trilioni 1.9 ni muhimu kwa wananchi kwa kuwa itaimarisha huduma za maji, kilimo, afya na hivyo kuleta maendeleo.

Shirika la Umeme (TANESCO) liliweka saini mikataba sita kwa ajili ya miradi 26 ya gridi imara na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iiliweka saini mikataba 14 kwa ajili ya miradi ya kupeleka umeme kwenye migodi midogomidogo na maeneo ya kilimo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news